Peter Isare Gasaya
Mkurugenzi Mkuu.

Ndugu mwekezaji,
Kwa niaba ya viongozi wenzangu ninakukaribisha katika kampuni yetu uweze kuwekeza fedha zako kwa kununua hisa za JATU PLC.

Jatu PLC ni kampuni ya kitanzania ambayo ilianzishwa tangu mwaka 2016 mwezi October, tarehe 20 ilipopata usajili wa kudumu kutoka BRELA.

Dhima kuu ya Jatu PLC ni kujenga afya na kutokomeza umaskini kwa kutumia rasilimali watu, kilimo na viwanda.

Jatu imejikita katika miradi ya kilimo, viwanda na masoko, na kwa kuwa Jatu Ina wanachama ambao ndo wateja wake wakubwa, imesajili saccos ambayo lengo kuu ni kuwakopesha wanachama wake mikopo ya maendeleo kwa riba ndogo na mikopo ya kilimo bila riba yeyote. Dhana hii imelenga kutokomeza umaskini kwa kuwawezesha wanachama wake mitaji yenye masharti nafuu na ili waweze kushiriki miradi ya kilimo itakayowezesha kampuni ipate malighafi za kutosha viwandani.

Kampuni kwa sasa inazalisha bidhaa za aina tatu ambazo ni; Mchele, Mafuta ya alizeti na unga wa mahindi wa dona na sembe kupitia viwanda vya Jatu ambavyo vipo kibaigwa, Dodoma na Kilombero, Morogoro. Hadi sasa zaidi ya watanzania milioni moja wananufaika na huduma zetu katika mikoa zaidi ya 15 Tanzania bara na visiwani. Tunazo ofisi za kutoa huduma zetu; Mwanza, Arusha, Dodoma, Mtwara, Manyara Kiteto, Morogoro, na Dar Es Salaam ambapo ndo ofisi kuu ya Jatu PLC.

Pia kuna Bidhaa zingine za chakula na Afya ambazo zinazalisha na wanachama kupitia fursa ya Balozi, hizi huandaliwa na balozi kama mzalishaji na kuuzwa katika masoko ya JATU na wanachama hupata gawio la faida kutokana na bidhaa hizo ambazo balozi ameziweka kwenye mfumo wetu.

Jatu ina mpango kabambe ujulikano kama maono ya mwaka 2022 (Jatu vision 2022) mpango huu umelenga kuboresha na kuimarisha miradi ya kampuni katika idara ya kilimo, viwanda na masoko; lengo hili likifikiwa tutaweza kuwahudumia watanzania zaidi ya million tano na kuweza kutokomeza umaskini kwa zaidi ya asilimia 75% ya watu hao.

Mtanzania anayejiunga Jatu anategemea kunufaika kwa njia kuu tatu:

1. Gawio la faida kwa kila hisa kila mwaka

2. Gawio la faida kila mwezi kutokana na manunuzi ya bidhaa na,

3. Kwa kushiriki miradi ya kilimo na kupitia mikopo ya Jatu Saccos.

Jatu inahitaji wawekezaji wa kununua hisa zake kwa sasa kupitia soko la hisa DSE kwa sababu kuu mbili:

1. Ili kutoa fursa kwa kila mtanzania aweze kuwa mmiliki wa kampuni hii; na

2. Ili kukuza mtaji wa kampuni uweze kufikia kiasi cha shiling bilion saba na nusu (7,500,000,000/=) kwa ajili ya kuimarisha viwanda hasa kiwanda cha kibaigwa kinachozalisha unga wa dona na sembe lakini pia mtaji huu utawezesha kampuni iweze kununua zana dhabiti za kilimo na hivyo kufanikisha kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa wanachama na watanzania watakao hitaji kujiunga Jatu.

Kumbuka; Jatu inalazimika kuwasaidia wakulima wafanye kilimo cha kisasa na inawapa uhakika wa masoko ili kuwaepusha wakulima kutoka mikono ya madalali lakini pia kuwezesha kampuni kupata malighafi za kutosha viwandani kwake ili mwisho wa siku mwanachama na mtanzania wa kawaida aweze kununua bidhaa za chakula kwa bei nafuu lakini ambayo inatengeneza faida kubwa kwa kampuni na kwa mteja kupitia gawio la faida la kila mwezi ambalo hutolewa kwa wateja wote wanaonunua bidhaa za chakula kupitia Jatu app.

Weka malengo na uifikie ndoto yako ya kumiliki kampuni kubwa ya Umma Tanzania kwa kujaza fomu pakua fomu yako kwa Kubofya hapa https://jatu.co.tz/fomu-maalumu-ya-kuomba-kumiliki-sehemu-ya-kampuni-ya-jatu-plc/ weka ahadi kuwa utanunua hisa wakati kampuni inaelekea soko la hisa mwaka huu. Hii Kitalaam inaitwa : Jatu initial public offering (IPO) kupitia Dar Es Salaam stock of exchange (DSE)

Zipo faida nyingi sana za kukufanya ununue hisa za Jatu PLC. Naamini utakuwa mwekezaji ndani ya Jatu PLC na mimi na timu yangu tumejiandaa kukupokea na kukuhudumia kwa unyenyekevu mkubwa.

Peter Isare
Founder and C.E.O
Jatu public limited company.
Let money work for you and not you working for money.

Shukrani Sana, Na karibu Sana Jatu.

Jatu tunasema;
“Jenga Afya Tokomeza Umasikini”.