JATU inaendesha na kusimamia miradi mbalimbali kwa kushirikiana na wanachama wake
Kilimo
Tunaendesha na kusimamia miradi mbalimbali ya kilimo. Pia tunatafuta mashamba na kuyafanyia utafiti na tunapojiridhisha ni maeneo mazuri kwa kilimo tunawashirikisha wanachama ili waweze kuyamiliki mashamba hayo.
Tunatumia mfumo wa masoko ya mtandao katika kuuza bidhaa zetu, pia kila mteja (mwanachama) anayefanya manunuzi ya bidhaa hizo kupitia mfumo wetu (JATU APP) hupata sehemu ya faida (gawio 10%) ya bidhaa husika kila mwezi.
Kampuni ya JATU imekuwa ikianzisha viwanda vidogo karibu na maeneo ya miradi yake ya kilimo na kununua mazao ya wakulima wake ambao ni wanachama wetu na kisha kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kupitia mifumo yetu ya masoko.
JATU kwa kuwa tuna wanachama wengi na ambao ni wajasaliamali, tumeanzisha Saccos maalumu ambayo haina riba kwa mkulima wa JATU na ina masharti nafuu ya kukopa kwa wakati. Lengo ni kuhakikisha mwanajatu hakosi mtaji.
Jenga Afya Tokomeza Umaskini ( JATU) PLC ni kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa kama kampuni ya umma (Public Limited Company) inayowaunganisha wakulima na kuwawezesha kulima kisasa na baada ya mavuno kampuni hununua mazao yote na baadaye kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa wanachama wa JATU kwa mfumo wa biashara ya mtandao (network marketing).
maono
Kuwa kampuni inayoongoza na inayolenga katika kuongeza lishe, usalama wa chakula na kumaliza umaskini barani Afrika
Misheni
Kutumia rasilimali watu katika kilimo, teknolojia ya usindikaji wa chakula na uuzaji wa bidhaa bora za chakula kwa wateja wanaopendelea kutumia mkakati wa uuzaji wa mtandao kumaliza umaskini na kutajirisha jamii na afya njema.
Washirika wetu
Tunafurahi kufanya kazi na maelfu ya washirika. Wale wanaofanya kazi na sisi ni pamoja na
Ungana Nasi
Wasiliana Nasi
Msaada rahisi na wa moja kwa moja. Tunahakikisha unapata majibu ya suala lolote kwa wakati.