BAR TO BAR NA PIERE LIKWIDI

BAR TO BAR NA PIERE LIKWIDI

BUKU TANO INATOSHA yazidi kuwa gumzo  kutokana na njia mbalimbali zinazotumika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na kunufaika kwa namna moja ama nyingine na fursa hii ya hisa.

Tulianza na MTAA KWA MTAA kampeni ambazo mpaka sasa bado zinaendelea kuwafikia wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.

BAR TO BAR ni kampeni nyingine  iliyobuniwa ili kuzidi kuwafikia wananchi ambapo mabalozi  wa BUKU TANO INATOSHA watakua wakizunguka katika bar tofauti kuhakikisha kuwa wanatoa elimu zaidi kuhusu hisa na kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kuingiza buku tano anafaidika na hisa hizi za JATU kwa kumiliki hisa 10 kwa bei chee yaani elfu 5000.

Kampeni hizi zilianza rasmi jana Tabata katika bar ya Kitambaa Cheupe ambapo balozi  wetu Piere Likwidi  alikua pale na timu nzima ya JATU ambapo mashabiki zake walipata nafasi ya kupiga picha nae na kuwajazisha fomu maalum za kununua hisa.

JATU PLC ni kampuni ya umma hivyo lengo na dhumuni kuu la kampeni hii ni kuhakikisha kuwa kila mtu anakua sehemu ya kampuni kwa kumiliki hisa ambapo kwa BUKU TANO unajipatia hisa 10 za JATU na kupata faida nyingine nyingi ndani ya JATU kama mikopo ya kilimo isiyokua na riba au mikopo yenye riba nafuu kupitia JATU SACCOS.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili