UFAFANUZI ZAIDI KUHUSU KUPATA WADHAMINI WA MCHAKATO WA SOKO LA HISA (UNDERWRITERS) KWA AJILI YA JATU PLC

Download UFAFANUZI ZAIDI KUHUSU KUPATA WADHAMINI WA MCHAKATO WA SOKO LA HISA

 Download TANGAZO MAALUM

UFAFANUZI ZAIDI KUHUSU KUPATA WADHAMINI WA MCHAKATO WA SOKO LA HISA (UNDERWRITERS) KWA AJILI YA JATU PLC

1. MAANA YA SOKO LA HISA NA MCHAKATO WAKUINGIA SOKONI:

Soko la hisa ni taasisi inayosimamia na kuratibu mchakato wa uuzaji na manunuzi ya dhamana za mitaji mfano hisa.
Kwa Tanzania kuna soko moja tu lenye dhamana hiyo, yaani Soko la Hisa la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Exchange, (DSE) hili ndo soko pekee linalohusika na kukuza mtaji kwa kuuza sehemu ya umiliki (HISA) kwa Umma.

Kabla ya kufikia hatua ya kuuza hisa katika soko hili, muuzaji huwa anaandaa nyaraka mbali mbali ambazo huwa zinasomwa na kupitishwa na mamlaka husika; kwaTanzania tunayo mamlaka ya masoko na mitaji ambayo ni taasisi ya serikali inajulikana kwa kifupi kama CMSA Yaani Capital Market and securities Authority.

Kampuni inayouza hisa lazima ithibitishwe na CMSA pamoja na DSE ndipo iruhusiwe kutangaza na kuuza hisa zake kupitia soko la mitaji la Umma. Moja ya nyaraka muhimu sana katika mchakato huu ni waraka wa matarajio Yaani PROSPECTUS.

Prospectus inaandaliwa na muuzaji na moja ya vitu inavyotakiwa kuelezea ni pamoja na; mkakati ambao kampuni itatumia kufanikisha kuuza hisa na faida ambayo mwanahisa wataitarajia kutokana na uwekezaji huo. JATU PLC tayar tumefanikiwa kuandaa waraka huu na tumeweza kupeleka maombi yetu kwa mamlaka husika Yaani DSE na CMSA ili waturuhusu kuuza hisa zetu kwa Umma kupitia soko la DSE.

2. USHAURI WA DSE NA CMSA;

Moja ya ushauri ambao ulitolewa na mamlaka zote mbili kwa maana ya DSE na CMSA baada ya kusoma nyaraka zetu zote; walishauri kwamba ni vyema tuwe na UNDERWRITERS Yaani kwa lugha rahisi ni wadhamini ambao wataweza

kuihakikishia mamlaka kwamba Jatu ikiingia sokoni ndani ya siku chache (si zaidi ya mwezi mmoja) itakuwa imeuza hisa zote na kukusanya mtaji wa TSHS. billion 7.5.

3. NI NANI ANAWEZA KUWA UNDERWRITER WA HISA?

Mtu yeyote mwenye pesa anaweza kuwa underwriter wa hisa za JATU, lengo la kuwa na underwriters ni kujiaminisha kwamba endapo wateja watakosa kipindi cha kuuza hisa muda tutakao pewa ukiisha basi huyu mdhamini (underwriters) anaweza kuzinunua hisa zote za JATU ili tupate mtaji wa kutekeleza mpango biashara wetu.

Kujiaminisha kuuza hisa katika soko la hisa ni jambo zuri kwa pande zote Yaani kwa mamlaka inayosimamia soko na kwa kampuni inayopeleka hisa sokoni; Kwani endapo kampuni itaenda soko la hisa bila kujihakikishia kwamba inaweza kuuuza hisa zote kwa wakati uliotengwa basi kuna uwezekano mkubwa kampuni hiyo kushindwa kukidhi vigezo na hivyo kutoruhusiwa kukusanya mtaji kutoka kwa umma, lakini pia inaleta picha mbaya kwa mamlaka zinazosimamia soko la hisa Kwani soko linaonekana kudorora na hivyo kutokuvutia wawekezaji wapya.

Underwriter (s) anaweza mtu mmoja au hata zaidi ya watu 1000 na unapokuwa underwriter haimanishi kwamba wewe tayar umenunua hisa, wewe utasuburi hadi watu wanunue zile ambazo zitabaki bila kununuliwa ndizo ambazo utaruhusiwa kununua.

Anaweza kujitokeza mtu au kampuni moja tu au 2 zenye mtaji mzuri zikadhamini mchakato huu kwa maandishi (kila mmoja anasema ni hisa kiasi gani aweza Nunua incase..) na wakasubir tukiingia sokoni wateja wetu wakanunua hisa zikabaki wao wanunue na ikitokea zimenunuliwa zote kwenye soko la awali basi wao hawatakuwa na hisa za kununua tena.

Kumbuka underwriters ni watu ambao wananunua hisa katika soko la awali baada ya hisa hizo kushindwa kununuliwa na wateja wa kawaida, na baada ya hapo kampuni inaorodhesha hisa zote katika soko, ambalo kitaalamu linajulikana kama SECONDARY MARKET, katika secondary market huwa wateja wanauza na kununua hisa kwa kadri wanavyoweza na kwa bei ya soko; hivyo mtu anaweza kununua hisa

wakati wa IPO (primary market) na akasubiri wakati wa soko la pili bei ikiwa imepanda akauza hisa zake na kurudisha fedha yake na hata kupata faida maradufu; swala la faida sasa inategemea na bei ya hisa kwa wakati wa kununua na wakati wa kuuza.

4. KWANINI JATU IMEAMUA KUANZA NA WANACHAMA WAKE KABLA YA KUTAFUTA WADHAMINI WENGINE WA NJE?

Uongozi wa Jatu unajivunia wanachama waliopo JATU. Uongozi unaamini kwamba shiling bilion saba na million mia tano (7,500,000,000/-) ambayo ndo jumla ya fedha tunayotegemea kuuza hisa kupitia soko la hisa ni pesa ndogo sana ambayo wanachama wa Jatu wanaweza kumudu; lakini pia uongozi wa JATU unaamini kwamba JATU ni kwa ajili ya watanzania wa kipato cha kawaida na lengo ni kuwawezesha waweze kumiliki kampuni kubwa ya kisasa na wafanye miradi jumuishi kama vile Kilimo, viwanda na masoko. Kwa sababu hizi uongozi umeona ni vyema kuanza na wanachama kwanza ili wao wajitokeze na kusema Utayari wao katika kununua hisa unakomea wapi? Yaani kwa mfano kama tunazaidi ya wanachama 10,000 na wote wakaamua kununua hisa za JATU maana yake ni kwamba bila kujali uwezo wa kila mmoja (tunajua tunatofautiana) lakini wastani wa kila mmoja akinunua angalau hisa za Tshs 750,000/= tutafikia malengo yetu bila kuhangaika na hao wadhamini.

Hivyo basi barua au tangazo lilitoka leo likihasisha wanachama waweze kuweka ahadi maana yetu ni kwamba tuwathibitishie mamlaka ya DSE na CMSA kwamba sisi wanachama wa JATU PLC tunaouwezo wa kununua hisa zote kwa bei ya Tshs 2500/= kwa kila hisa moja pindi dirisha la kuuza hisa litakapofunguliwa. Na uongozi wa jatu utaorodhesha majina yenu yote pamoja na kiasi mlicho ahidi tutawatumia mamlaka husika nao watajiridhisha ili watupangie ratiba ya kuingia sokoni.

Itambulike kwamba swala hili ni la hiari kabisa na wala hautakiwa kutoa pesa zako na kuzilipa JATU, sisi tunataka tu utuhakikishie kwamba wewe ni miungoni mwa wanachama ambao watanunua hisa, na tujue ni hisa za thamani ya kiasi gani; kitaalamu hapa tutakuwa tunajenga kitabu cha wawekezaji wapya (book building). Pia ikumbukwe kwamba utaratibu huu hauathiri umiliki wako wa awali kwa maana ya kwamba kama ulishanunua hisa za JATU hapo nyuma haimanishi kwamba zile hisa

hazitambuliki, hisa zako zinatambulika na tayari orodha hiyo ipo katika mamlaka husika. Kwa sasa tunaongelea hisa mpya ambazo tunatarajia kuuza hivi karibuni kupitia soko la DSE na unaruhusiwa pia kununua zaidi kama unao mtaji.

5. NI KWANINI UNUNUE HISA ZA JATU PLC?

Wengi wenu mtajiuliza, je kuna umuhimu gani wa kununua hisa za JATU, nataka nikuhakikishie kwamba katika historia ya nchi yetu kwa mara ya kwanza imetokea kampuni ambayo inajibu hoja zote za watanzania kuhusu kupambana na umaskini, waasisi wa JATU waliamua kuanzisha kampuni hii na kuifanya iwe ya Umma kwa sababu waliamini na wanaamini ni suluhisho la umaskini na inatoa kipato kwa kila Mtanzania. Pamoja na kusudi hilo; ukinunua hisa za JATU ni tofauti na hisa zingine ulizozoea kwa sababu;

  1. Mbalinagawiolafaidakilamwaka(dividend),JATUinawasaidiawakulimakwa kuwatafutia mashamba, kuwapa wataalamu wa kilimo, kujenga miundombinu ya kisasa na kutoa mkopo wa kilimo usio na riba kwa mkulima; na ili uwe mkulima wa JATU ni lazima uwe na hisa angalau 400.
  2. Tunao mfumo wa mabalozi ambao wanasambaza bidhaa za JATU kwa kuwauzia wateja wa JATU walio karibu nao, balozi anapata faida kubwa zaidi kutokana na Mfumo wa JATU na gawio la faida la kila mwezi; ili uwe balozi wa JATU utalazimika kuwa na hisa angalau 400.
  3. Lakini pia JATU inamfumo wa masoko ambao unawezesha watu wanununue bidhaa na kuuza kupitia mtandao wake, wewe kama ni mjasiriamali utaruhusiwa kuuza bidhaa zako kwa wanachama wa JATU, hutopata shida ya soko, lakini ni lazima pia uwe na hisa JATU
  4. Kubwa zaidi ni kwamba JATU inahuduma ya kifedha ambapo tunatoa mikopo kwa wanachama wetu na hawa wanachama ni lazima wawe wanahisa.

Hivyo basi; kutokana na sababu Tajwa hapo juu; kila Mtanzania mwenye nia ya maendeleo analazimika kununua hisa za JATU ili apate fursa hizo; tunaamini kwamba wapo wengine ambao watashindwa kununua hisa wakati huu wa IPO lakini hiyo ni fursa Kwa wale ambao mtanunua hisa nying, kwani mtaweza kuuza hisa zenu kwa wageni watakao kuja kwa bei mtakayotaka wenyewe hapo badae, na hii itawawezesha pia kukuza kipato chenu. Amini usiamini kuna kila dalili inaonesha

kwamba hisa za JATU zitakuwa zikipanda bei na wengi wenu mtatajirika kutokana na hisa mtakazo kuwa nazo JATU PLC.

MWISHO:

Kuhusu kuwa underwriters nayo pia ni fursa, kama wewe ni mtu binafsi au taasisi ambayo inadhani kwa namna moja au nyingine unaweza kuthamini hisa hizi pia tunakukaribisha wasiliana nasi ili tuweze kuweka makubaliano bayana ya kisheria na wewe utakuwa underwriter wa hisa za JATU, Kumbuka ukiwa underwriter kuna faida au ofa unayopata ambayo ni ya upendeleo kutokana na makubaliano tutakayo ingia.

Napenda kuwashukuru kwa mapenzi mema mliyonayo juu ya Nchi yetu na sasa mmeamua kuwekeza kupitia JATU, nawashauri mfanye maamuzi sahihi baada ya kutathimini swala hili na kujiridhisha, tafadhari usitoe pesa yeyote kwa yeyote yule kwa kipindi hichi; zoezi hili sio la kuuza hisa bali ni la kutaka kujiridhisha kama tunao wanunuzi wa hisa za JATU. Weka ahadi yako kwa kadri uwezavyo; wasilisha katika ofisi husika, baada ya hapo kaa usubiri ratiba ya soko la hisa tutawatangazia hivi karibuni na wewe utaenda kununua hisa zako kwa mawakala tutakao watangazia.

MUHIMU:
Unaruhusiwa kumshirikisha rafiki yako habari hizi, hata kama sio mwanachama kwa sasa lakini anayo nia ya kuwekeza JATU, Mpe habari njema.. hata walio nje ya Tanzania pia tunawakaribisha, iwe taasisi ya Umma, vikundi, kampuni au watu binafsi njoo tuungane tuokoe Nchi yetu kwa kupambana na umaskini. Kumbuka tunauza hisa kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika kilimo ili tuasaidie watu wengi Zaidi na Kujenga kiwanda cha kisasa katika mkoa wa Manyara wilaya ya Kiteto kwa ajili ya kuzalisha unga wa mahindi na mafuta ya alizeti ambavyo ni chakula muhimu kwa maisha yetu sisi wanadamu.
___________________________________

Imeandikwa na;
Peter Isare
Founder and CEO
JATU PUBLIC LIMITED COMPANY 16.10.2019

JATU – JENGA AFYA TOKOMEZA UMASKINI

TOLEO LA NNE: HAKIKI ORODHA YA WANAHISA WA JATU PLC

Download kwa kuminya Jatu List ya Wanahisa hapa chini {UPDATED}

PAKUA ORODHA YA WANAHISA WA JATU PLC

Rejea Tangazo la Tarehe 09 septemba 2019 kuhusiana na orodha ya wanahisa wa Jatu Plc

TANGAZO

 

_____________________________________________________________________

Habari

Tarehe 10.09.2019 tunategemea kutoa orodha ya wanahisa wa JATU PLC ambao walinunua hisa za ndani na walikubaliana na utaratibu wa kuchangia Tshs. 30,000/= kwa ajili ya zoezi la soko la hisa (DSE). Kama ukiona jina lako halipo ujue haukukidhi vigezo vya kuwa mwanahisa wa JATU PLC na hivyo unapaswa kufika ofisini kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kurejeshewa pesa zako ulizokuwa unatarajia kununua hisa za Jatu. Wale ambao mtaona majina yenu kila mmoja ataandikiwa barua na utatakiwa kufika ofisini au kutuma Barua pepe yako kwenda ipo@jatu.co.tz ili tukutumie barua yako ya kukutambua rasmi kama mwekezaji wa awali wa JATU PLC kabla ya Initial Public Offering (IPO). Majina yote yatawekwa kwenye tovuti rasmi ya Kampuni.

JATU PLC: YAPATA MUALIKO WIZARA YA KILIMO

 

Jatu Plc imepata nafasi ya kualikwa na Wizara ya Kilimo katika mkutano wa siku mbili (29.08.2019 – 30.08.2019), Mkutano huo unawakutanisha wafanyabiashara na wadau wa nafaka nchini pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika tasnia hiyo ya nafaka na jinsi ya kuzitumia ikiwa ni pamoja na Masoko.

Jatu katika mkutano huo inawakilishwa vyema na Eng. Dr. Zaipuna Obedi Yonah ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Jatu Plc.

Jatu inatoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa mualiko huo, na kuwaahidi wanachama wetu kuwa, tutaitumia fursa hii vyema katika kutanua wigo wa biashara yetu ya mazao ya nafaka na Masoko kwa ujumla ili kufikia lengo letu la kujenga Afya na kutokomeza umaskini kupitia Kilimo, Viwanda na Masoko.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE ABARIKI SAFARI YA JATU KUELEKEA D.S.E

Na: Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Temeke ndugu, Felix Lyaniva amesema kuwa, kitendo cha kampuni ya Jatu Plc kuamua kuelekea kwenye Soko la Hisa D.S.E ni jambo nzuri na analiunga mkono na anaamini litachangia kuondoa umasikini kwa jamii na kukuza uchumi kwa ujumla.

Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu wa ziada wa wanahisa uliofanyika tarehe 01.06.2019 jijini Dar es Salaam, ambapo ndugu; Lyaniva alisema kuwa, ili safari hiyo ya kuelekea soko la hisa iwe nzuri ni vyema wanachama wote wakashirikishwa kufanya maamuzi katika hatua hiyo ya kuelekea soko la hisa ili kuepuka manung’uniko ya wanachama kutoshirikishwa katika maamuzi hayo.

“Nimeambiwa mnakwenda kwenye soko la hisa, ninaomba nitoe maelekezo yafuatayo; Kabla hamjaenda kwenye soko la hisa ninataka na ninaelekeza wanahisa wote mridhie. Wazo limekuja , limetolewa mnaenda kwenye soko la hisa jambo ambalo ni nzuri, jambo ambalo ni la kuondoa umasikini, lakini baada ya hapo kusiwe na manung’uniko nataka wote kwa kauli moja mseme twendeni huko na mimi niwashauri nendeni kwenye soko la hisa huko ni kuzuri zaidi

alisema mkuu wa wilaya Temeke ndugu; Lyaniva.

Aidha, ndugu;Lyaniva amewataka wanachama wa kawaida wa jatu ambao bado hawajaanza kuwekeza kwa kununua hisa za Jatu kuanza kushawishika kufanya hivyo, kwani ni biashara nzuri kwa kila mtu hata kwa wale wanaoelekea kustafu.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa wilaya ya Temeke amewataka wanajatu kuwa kitu kimoja na kujitahidi kuhudhuria vikao vinavyoitishwa, kwani mikutano hiyo ndio sehemu pekee ya kutatua changamoto na kumaliza migongano mbalimbali katika kampuni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Jatu Plc, ndugu; Peter Isare, akizungumza kabla ya wanahisa wa kampuni hiyo kufanya uchaguzi wa bodi mpya ya wakurugenzi ambayo pia ilichaguliwa kupitia mkutano huo, alisema kuwa, ni vyema wanabodi watakaopata nafasi hiyo ya kuchaguliwa wakatambua dhamira ya Jatu, ambayo ni kuisaidia jamii ya Watanzania katika kutokomeza umasikini kupitia kilimo, viwanda na masoko na hivyo kuwasihi kuitumikia jatu kwa uaminifu na weledi, huku wakitanguliza maslai ya wanajatu mbele na si maslai ya mtu mmoja mmoja au ya kwao binafsi.

Mbali na hayo, kupitia mkutano huo wanachama walipata nafasi ya kupata elimu kuhusu masuala ya hisa kutoka Kampuni ya Archy Financial Lt.d iliyoko chini ya ndugu, Richard Manamba, ambaye aliwaeleza wanachama wa jatu kuhusu taratibu za usajili wa kampuni katika soko la hisa pamoja na faida za kampuni kuingia katika soko hilo la hisa na manufaa anayoyapata mwanachama mmoja mmoja endapo kampuni itasajili hisa zake katika soko la hisa la DSE.