JATU PLC: YAPATA MUALIKO WIZARA YA KILIMO

 

Jatu Plc imepata nafasi ya kualikwa na Wizara ya Kilimo katika mkutano wa siku mbili (29.08.2019 – 30.08.2019), Mkutano huo unawakutanisha wafanyabiashara na wadau wa nafaka nchini pamoja na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika tasnia hiyo ya nafaka na jinsi ya kuzitumia ikiwa ni pamoja na Masoko.

Jatu katika mkutano huo inawakilishwa vyema na Eng. Dr. Zaipuna Obedi Yonah ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Jatu Plc.

Jatu inatoa shukrani kwa Wizara ya Kilimo kwa mualiko huo, na kuwaahidi wanachama wetu kuwa, tutaitumia fursa hii vyema katika kutanua wigo wa biashara yetu ya mazao ya nafaka na Masoko kwa ujumla ili kufikia lengo letu la kujenga Afya na kutokomeza umaskini kupitia Kilimo, Viwanda na Masoko.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE ABARIKI SAFARI YA JATU KUELEKEA D.S.E

Na: Mwandishi Wetu

Mkuu wa Wilaya ya Temeke ndugu, Felix Lyaniva amesema kuwa, kitendo cha kampuni ya Jatu Plc kuamua kuelekea kwenye Soko la Hisa D.S.E ni jambo nzuri na analiunga mkono na anaamini litachangia kuondoa umasikini kwa jamii na kukuza uchumi kwa ujumla.

Hayo ameyasema alipokuwa akizungumza katika mkutano mkuu wa ziada wa wanahisa uliofanyika tarehe 01.06.2019 jijini Dar es Salaam, ambapo ndugu; Lyaniva alisema kuwa, ili safari hiyo ya kuelekea soko la hisa iwe nzuri ni vyema wanachama wote wakashirikishwa kufanya maamuzi katika hatua hiyo ya kuelekea soko la hisa ili kuepuka manung’uniko ya wanachama kutoshirikishwa katika maamuzi hayo.

“Nimeambiwa mnakwenda kwenye soko la hisa, ninaomba nitoe maelekezo yafuatayo; Kabla hamjaenda kwenye soko la hisa ninataka na ninaelekeza wanahisa wote mridhie. Wazo limekuja , limetolewa mnaenda kwenye soko la hisa jambo ambalo ni nzuri, jambo ambalo ni la kuondoa umasikini, lakini baada ya hapo kusiwe na manung’uniko nataka wote kwa kauli moja mseme twendeni huko na mimi niwashauri nendeni kwenye soko la hisa huko ni kuzuri zaidi

alisema mkuu wa wilaya Temeke ndugu; Lyaniva.

Aidha, ndugu;Lyaniva amewataka wanachama wa kawaida wa jatu ambao bado hawajaanza kuwekeza kwa kununua hisa za Jatu kuanza kushawishika kufanya hivyo, kwani ni biashara nzuri kwa kila mtu hata kwa wale wanaoelekea kustafu.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa wilaya ya Temeke amewataka wanajatu kuwa kitu kimoja na kujitahidi kuhudhuria vikao vinavyoitishwa, kwani mikutano hiyo ndio sehemu pekee ya kutatua changamoto na kumaliza migongano mbalimbali katika kampuni.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Jatu Plc, ndugu; Peter Isare, akizungumza kabla ya wanahisa wa kampuni hiyo kufanya uchaguzi wa bodi mpya ya wakurugenzi ambayo pia ilichaguliwa kupitia mkutano huo, alisema kuwa, ni vyema wanabodi watakaopata nafasi hiyo ya kuchaguliwa wakatambua dhamira ya Jatu, ambayo ni kuisaidia jamii ya Watanzania katika kutokomeza umasikini kupitia kilimo, viwanda na masoko na hivyo kuwasihi kuitumikia jatu kwa uaminifu na weledi, huku wakitanguliza maslai ya wanajatu mbele na si maslai ya mtu mmoja mmoja au ya kwao binafsi.

Mbali na hayo, kupitia mkutano huo wanachama walipata nafasi ya kupata elimu kuhusu masuala ya hisa kutoka Kampuni ya Archy Financial Lt.d iliyoko chini ya ndugu, Richard Manamba, ambaye aliwaeleza wanachama wa jatu kuhusu taratibu za usajili wa kampuni katika soko la hisa pamoja na faida za kampuni kuingia katika soko hilo la hisa na manufaa anayoyapata mwanachama mmoja mmoja endapo kampuni itasajili hisa zake katika soko la hisa la DSE.

MKUTANO WA WANAHISA WA JATU

Leo ilikuwa siku ya kikao cha dharura cha wanahisa wa Jatu PLC, Ajenda kuu tuliyojadili ni kuhusu mkutano mkuu wa wanahisa wa mwaka 2018 (Annual general Meeting).

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa jatu kufanya mkutano (2nd Annual General Meeting), tumekubaliana mkutano huu utafanyika tarehe 27.04.2019 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni. Eneo na ukumbi ni katika ofisi kuu za Jatu PLC zilizopo ndani ya viwanja vya sabasaba Maonesho; kilwa road, Temeke.

Mkutano mkuu utajadili miradi, na Bajeti ya kampuni kwa mwaka ujao na huku ukihakiki mapato na matumizi ya mwaka uliopita.

Wanaoruhusiwa kushiriki ni wanahisa wote wa Jatu PLC ambao wanahisa hamsini au zaidi. Coupon za kushiriki mkutano huu zinapatikana katika app ya Jatu kwa gharama ya tshs. 5000/=, kila mwanahisa anashauriwa kulipia coupon yake kabla ya tarehe 05.04.2019 ili kuruhusu mambo mengine ya maandalizi yaendelee. Hata hivyo Tarehe 06.04.2019 tutatoa tangazo rasmi la mwaliko wa mkutano huu.

Kwa wale ambao wanapenda kuwa wanahisa wa jatu na wanahitaji kushiriki katika kikao hichi, wanashauriwa kununua hisa za jatu kupitia app ya jatu ambayo ipo Playstore.

JATU_kilimo | Viwanda | Masoko | Mikopo

 

KILIMO CHA MAHARAGWE KILINDI TANGA

 

Habari kutoka kwa mkurugenzi wa Jatu Ndugu Peter Isare
Kama mlivyoona jana baada ya kutembelea Eneo la KILINDI, nilitoa ushauri kama kuna mtu anatamani kulima maharagwe katika mkoa wa Tanga eneo la Kilindi aungane na mimi msimu ndo unaelekea kuanza ili tujaribu tuone.

Kwa kifupi tu; kilimo cha maharagwe kina faida kubwa sana ukilinganisha na mazao mengine. Jatu ipo kwa ajili ya kuhakikisha unashiriki katika fursa za kilimo nyingi kadri iwezekanavyo. Mashamba yapo mazuri yanapatikana kwa kukodi. Gharama ni nafuu; Tunayo Jatu Saccos Ltd itakusaidia mkopo wa kilimo bila Riba ili kupunguza makali na wewe utalipia mkopo wako baada ya mavuno. Soko la maharagwe hasa yale ya Njano ni kubwa sana na bei ni nzuri siku zote.

Kama wewe ni mwenye Nia; bonyeza link hapa chini uweze kujiunga na group hili uweze kupata maelezo zaidi.????????

Open this link to join my WhatsApp Group: https://chat.whatsapp.com/JcRDyym3qKVIG5iO2iTPTA

Mwisho wa kujiunga na group hili ni Jumapili jion tarehe 17.03.2019 baada ya hapo link itafungwa na tutaanza kutoa maelezo ya gharama na vigezo kuhusu kilimo hichi. Mshirikishe na mwenzako hata kama hajajiunga jatu huu ndo muda wa kujiunga na kushiriki fursa????

JATU KILIMO | VIWANDA | MASOKO | MKOPO