JATU PLC: SEMINA OFISI ZA KILIMO MKOA WA MOROGORO

Na Mwandishi wetu:

Idara ya Masoko ya Jatu plc leo imepata wasaa wa kutembelea mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mary Chulle ambaye ni mkuu wa idara hiyo, na kupata fursa ya kutembelea ofisi za idara za kilimo, uvuvi na ufugaji manispaa ya Morogoro. eneo la Boma Kitope Road, wamepata wasaa wa kuongea na watumishi hao kuhusu fursa zote za JATU na wote wameonesha kufurahishwa nazo, haswa katika kuwaeleza kuhusu Jatu wanavyofanya kilimo na kumkwamua mkulima katika kuepukana na madalali na kupata soko la uhakika ukilima na JATU PLC.

watumishi hao wameweza kujiunga na kufurahia bidhaa za JATU ambazo zinatokana na kilimo kinachofanywa na JATU na wanachama wake, Aidha Mary ameweza kuelezea kuwa Jatu bado ipo katika mikakati ya kuweza kuifikia Tanzania katika wilaya zake mbalimbali kwa nia ya kuwapa watanzania wote habari njema zinazohusiana na JATU, ili waweze kujikwamua kwenye maswala ya kulima na waweze kutumia bidhaa zenye faida kutokana na kula au kutumia bidhaa za JATUna  kupata malipo ambayo ni sehemu ya faida ya bidhaa ambazo zinazalishwa na JATU.

Leave a Reply

Funga menu
English
Kiswahili English