JATU PLC: YAPATA MUALIKO WIZARA YA KILIMO

Safari ya Kiteto

Tarehe 10.09.2019 tunategemea kutoa orodha ya wanahisa wa JATU PLC ambao walinunua hisa za ndani na walikubaliana na utaratibu wa kuchangia Tshs. 30,000/= kwa ajili ya zoezi la soko la hisa (DSE). Kama ukiona jina lako halipo ujue haukukidhi vigezo vya kuwa mwanahisa wa JATU PLC na hivyo unapaswa kufika ofisini kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kurejeshewa pesa zako ulizokuwa unatarajia kununua hisa za Jatu. Wale ambao mtaona majina yenu kila mmoja ataandikiwa barua na utatakiwa kufika ofisini au kutuma Barua pepe yako kwenda ipo@jatu.co.tz ili tukutumie barua yako ya kukutambua rasmi kama mwekezaji wa awali wa JATU PLC kabla ya Initial Public Offering (IPO). Majina yote yatawekwa kwenye tovuti rasmi ya Kampuni.

Leave a Reply

Funga menu
English
Kiswahili English