JATU Agriculture

Kampuni ya Jatu inaendesha na kusimamia miradi mbalimbali ya kilimo tukiwashauri wanachama wetu kumiliki au kukodi mashamba makubwa na yenye rutuba ambayo hukubali mazao ambayo, kampuni huyahitaji katika uzalishaji wa bidhaa zetu. Hadi sasa JATU kwa kushirikiana na wanachama wetu tumefanikiwa kumiliki mashamba makubwa yanayopatikana mkoani ManyaraMorogoro, Rukwa, Njombe, na Tanga.

In Manyara region Kiteto district JATU is running a maize and sunflower farming project, where more than 2000 acres have already been cultivated, with the expectation of delivering 5,000 acres of the crop by 2022.

Mkoani Morogoro wilayani Kilombero Jatu imejikita katika kilimo cha mpunga, ambapo hadi kufikia sasa ekari zadi ya 2500 zimeshalimwa, huku kampuni ikiendeleza uwekezaji zaidi katika kilimo hicho ili ifikapo mwaka 2022 kuwe na ekeri takribani 5000 zitakazokuwa zimelimwa zao hilo la mpunga.

Kampuni ya JATU pia imejikita katika kilimo cha matunda kama parachichi mkoa wa Njombe na Machungwa yanalimwa na kampuni ya JATU PLC mkoa wa Tanga katika wilaya ya Handeni na wilaya muheza.

Alizeti na mahindi vinalimwa wilayani kiteto mkoa wa Manyara. Zao la maharage llinalimwa wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga ambapo mpaka sasa hekari Zaidi ya 2500 zimeshalimwa.

In addition, our plan JATU is to ensure that we establish farms in every district here in Tanzania and we will provide these farms with irrigation infrastructure, while accompanied by factories in it.

FAIDA ZA KULIMA NA JATU

  • Uhakika wa mashamba mazuri kwa ajili ya mazao unayotaka kulima
  • Uhakika wa usimamizi wa kitaalamu katika kilimo.
  • Uhakika wa maghala ya kuhifadhi mazao yako bure.
  • Uhakika wa matumizi bora ya teknologia, zana na pembejeo bora za kilimo.
  • Uhakika wa soko kwa mazao yako.
  • Uhakika wa mkopo wa kilimo usio na riba.

VIGEZO VYA KUSHIRIKI KILIMO NA JATU.

  1. Uwe umejiunga na kampuni ya JATU kwa kupata namba ya uanachama.
  2. Uwe na hisa 50 kwa kila ekari kuanzia ekari 1 hadi 49 yaani uwiano wa 1:50, pia hisa 500 kwa kila ekari kuanzia ekari 50 na kuendelea yaani kwa uwiano wa 1:500
  3. Uwe umejiunga na JATU SACCOS ili kupata mkopo wa kilimo bila riba.
Funga menu
English
Kiswahili English