Jatu Plc tunatoa uhakika wa soko kwa kununua mazao ya wakulima wote ambao wamelima chini ya usimamizi wetu na kuchakata mazao hayo katika viwanda vyetu na  baada ya hapo tunatengeneza bidhaa ambazo zina nembo ya JATU, baadhi ya bidhaa hizo ni kama zifuatazo;

 1. Maharage.
 2. Mchele.
 3. Mafuta ya kula (jatu alizeti).
 4. Unga wa sembe pamoja na dona.
 5. Mahindi ya kande.
 6. Karanga.

Mtu anayejiunga na kampuni ya JATU ni lazima akubali kuwa miongoni mwa wanunuzi(mwanachama mteja) wa bidhaa zinazoandaliwa na JATU ili aweze kunufaika zaidi yaani KULA ULIPWE, fursa hii inatokana na gawio la faida kutokana na manunuzi ya bidhaa anayoyafanya mwanachama.

JATU pia imekuwa ikitoa fursa ya masoko ya bidhaa za wajasiriamali wengine (JATU BALOZI) ambao ni wanachama kwa kuruhusu bidhaa zao kuuzwa kupitia mfumo wa Jatu (JATU MARKET) endapo bidhaa husika itakuwa na ubora na kuhitajika sokoni. (Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0758396767 au fika katika ofisi zetu).

Mfumo wa JATU (JATU MARKET) humpatia mwanachama (mteja) nafasi ya kufanya manunuzi ya bidhaa za kila siku kwa kuweka oda kupitia mfumo huo na kisha kufikishiwa hadi sehemu alipo (nyumbani, kazini) pindi mteja anapokamilisha malipo.

Ili kufanikisha kufanya manunuzi au oda kupitia mfumo wa JATU mwanachama anapaswa kufuata taratibu zifuatazo:-

 1. Kupakua App ya JATU MARKET kupitia playstore kwa watumiaji wa android au Appstore kwa watumiaji wa Iphone.
 2. Utakuta kitufe cha kujisajili na kuingia, kama haujajisajili utajisajili kwa kujaza taarifa zako sahihi kulingana na maelekezo na kama umejisajili,
 3. Ingia katika mfumo wa JATU kwa namba yako ya uanachama yenye utambulisho wa AA-XXXX, AB-XXXX au AC-XXXX.
 4. Baada ya kuingia, itakupeleka nyumbani utaweza kuona maduka mbalimbali, utachagua duka kulingana na mkoa uliopo kwa ajili ya kufanya manunuzi.
 5. Utaweza kuona bidhaa zilizopo katika duka husika, utabonyeza kitufe cha ona zote, kisha utachagua bidhaa ambazo unahitaji.
 6. Ukishachagua bidhaa utaona kiasi na idadi ya bidhaa zilizopo, chini yake utaona ujazo(lita) au uzito(kg), upande wa kulia utaona batani mbili, moja ya kujumlisha na nyingine ya kutoa.
 7. Ukibofya alama ya kujumlisha inaongeza idadi ya bidhaa pamoja na bei na kutoa unapunguza idadi ya bidhaa pamoja na bei, baada ya apo utaweka kapuni, utabofya endelea.
 8. Utabofya kitufe cha weka oda,utachagua kati ya safirisha bidhaa au usisafirishe bidhaa, kama utasafirisha bidhaa utaandika sehemu ambayo unahitaji upelekewe bidhaa,kisha utachagua eneo na utabofya alama ya tick kuendelea.
 9. Itaonyesha gharama ya bidhaa jumlisha na ya usafirishaji, kisha weka oda.
 10. Oda ikishatumwa utapokea ujumbe mfupi wa maneno (meseji) kupitia simu yako ya mkononi inayotambulika katika mfumo wa JATU,mfano wa ujumbe ni kama ufuatayo ”Bill namba AB-2075-SB-0001 yenye kumbukumbu no. 213505 imefanikiwa kutengenezwa Tafadhali lipia jatu Sh. 5000/= ili uweze kuletewa mzigo” ujumbe huo unamuonesha mteja husika kwamba amefanikiwa kuweka oda na anapaswa kulipia kiwango kilichoainishwa kwenye ujumbe husika.
 11. Baada ya ujumbe huo mteja utapaswa kuingia menu ya Tigo Pesa, Airtelmoney au M-Pesa na ufuate taratatibu zifuatazo:-
 • Nenda lipa kwa M-Pesa, Airtel money au Tigo Pesa
 • Chagua lipa kwa M-Pesa, Airtel money au Tigo Pesa
 • Then select the section to fill in the business number
 • Enter the business number correctly, which is 370033
 • Then write down the reference number you received in the text message (text message) via your mobile phone.
 • Baada ya hapo utapokea ujumbe mara tu baada ya kufanya malipo ukiachana na ujumbe wa Tigo Pesa, airtel money au M-Pesa utapokea ujumbe mfupi wa maneno (sms) kutoka JATU utakaosomeka hivi; “Hongera malipo yamefanikiwa Bill no AB-2075-SB0001 yenye kumbukumbu no 213505 imefanikiwa kulipwa mzigo utakuja hivi karibuni” Hiyo sms ni kama risiti kwako mteja.
Funga menu
English
Kiswahili English