TAARIFA MAALUMU (WANACHAMA WOTE WA JATU PLC)

TAARIFA MAALUMU (WANACHAMA WOTE WA JATU PLC)

Ndugu wanachama na wote mnaotegemea kuwa wanachama wa JATU PLC, tunapenda kuwajulisha kwamba maandalizi ya kilimo kwa msimu wa 2022-2023 tayari yameanza, zoezi linaloendela sasa hivi ni la kulipia mashamba na kuweka akiba ili ifikapo mwezi October tuweze kuanza zoezi la kulima. Uongozi wa JATU unapenda kutoa taarifa na utaratibu mpya utakaotumika katika uwekezaji wa kilimo na ufugaji kwa msimu wa 2022-2023 kama ilivyoelezewa katika mkutano wa kilimo uliofanyika tarehe 02.04.2022 katika ukumbi wa Blue Pearly Hotel, Ubungo Plaza, Dar es salaam.

  1. Kwa msimu wa mwaka 2022-2023 wanachama watakao shiriki mradi wa kilimo cha Mpunga, Mahindi, Maharage na Alizeti ni wale tu walio na mashamba ya kudumu (kununua) katika mradi wa JATU na wale walio bahatika kukodi wakati wa ofa ya kufunga na kufungua msimu iliyotangazwa mwishoni mwa mwezi Machi, 2022. Wanachama hao orodha yao imeandaliwa na inapatikana katika tovuti yetu ya www.jatukilimo.com, kila mwanachama anashauriwa kuangalia namba yake ya uanachama ili aweze kuhakiki idadi ya ekari zake na aanze kuweka akiba JATU Saccos Ltd kwa mujibu wa kanuni za jatu saccos.
  2. Zao la SOYA ndo mradi pekee ambao wanachama wanaruhusiwa kukodi mashamba na kulima kwa msimu wa mwaka 2022-2023. Tunawashauri wote ambao wanatamani kulima na JATU na hawana mashamba ya kudumu katika mazao mengine yanayolimwa na kampuni, waweze kuwahi nafasi ya kukodi mashamba katika zao la Soya. Soya ni zao ambalo linalimwa katika mkoa wa Rukwa na lina soko na bei ya uhakika, JATU tunataka kuwa wazalishaji wakubwa wa zao la soya na hivyo tunawashauri wanachama kukodi ekari nyingi zaidi ili tuweze kufikia lengo. Gharama na utaratibu wa kukodi ekari Kwa ajili ya zao la soya tumewawekea katika app ya JATU MARKET inayopatikana Playstore na AppStore.
  3. Mradi wa parachichi utaendelea kupokea wanachama wapya kwa msimu wa 2022/2023. Mashamba yanapatikana katika app ya JATU Market. Kwa wanachama walionunua mashamba na kuweka akiba orodha yao inapatikana katika tovuti ya JATU kilimo. Pia kuhusu mradi wa chungwa kampuni kwa sasa imefikia ukomo katika kupokea wanachama wapya, kwa wanachama waliolipia mashamba na kuweka akiba orodha yao inapatikana kwenye tovuti kila mmoja ahakiki taarifa zake.
  4. Mradi wa ufugaji wa muda mfupi batch 1-5 sasa umefikia ukomo, Tunategemea kuendelea na batch 6 mwezi November baada ya kukamilika kwa batch 5 mwezi October 2022. Hata hivyo, ili kuweza kuwa na uzalishaji Bora wa nyama, kampuni imeanza mradi wa kudumu wa ufugaji wa ng’ombe aina ya Borani (parent stock) ambao watakua wazazi wakuzaa ndama na badae hao ndama kuingizwa katika unenepeshaji (feedlots). kampuni inawakaribisha wanachama wanaopenda kuwekeza katika ng’ombe wa kudumu ambao wanategemewa kudumu kwa kipindi Cha miaka 10 waweze kushiriki; gharama na utaratibu wa kulipia ng’ombe hao unapatikana kupitia app ya JATU market na tovuti ya jatu kilimo. Pia wanachama walionunua mashamba kwa ajili ya ufugaji orodha yao imeorodheshwa kupitia tovuti yetu kila mmoja na ahakiki taarifa zake.

Mwisho, tunawakumbusha kwamba tarehe 27 – 29 mwezi huu tutakuwa kiteto katika shamba letu na wanachama wote ambao wanamashamba kiteto mnatakiwa kujiandaa na kulipia safari hiyo mapema iwezekanavyo ili maandalizi yafanyike kwa wakati na baada ya kutoka kiteto tutatangaza ratiba ya kwenda katika shamba la parachichi na mazao mengine. Endelea kufatilia vipindi na matukio ya JATU kupitia kurasa zetu na mitandao ya kijamii, tovuti na TV yetu ya mtandaoni (Youtube) Yaani JATU TALK TV, kwa maelezo zaidi Wasiliana nasi kupitia; 0758 396 767 au fika katika ofisi zetu zilizo karibu na wewe.

Tunawatakia Eid Njema.

“Jatu, Jenga Afya Tokomeza Umaskini”

Leave a Reply

Funga menu
English
Kiswahili English