Factories

Kampuni ya Jatu ina  viwanda karibu na miradi yetu ya kilimo, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa malighafi.

Kupitia viwanda hivyo kampuni hununua mazao ya wakulima ambao ni wanachama wetu na kuandaa bidhaa ambazo tunaziuza kupitia JATU MARKET kwa mlengo wa masoko ya kimtandao (Network Marketing). Hivyo mwanachama wa Jatu ambaye amelima na kampuni hupata nafasi ya mazao yake kuuzwa na kutumika kama malighafi katika viwanda vyetu.

JATU imejenga kiwanda cha kuzalisha unga katika mji mdogo wa Kibaigwa wilaya ya kogwa mkoa wa Dodoma. Kupitia kituo hichi kampuni inazalisha unga wa mahindi wa dona na sembe na kufungasha katika mifuko maalumu yenye nembo ya kampuni.

Pia kiwanda cha kukamua mbegu za alizeti na kuzalisha mafuta ya kupikia yajulikanayo kama mafuta ya alizeti ambayo hayana lehemu (cholesterol) na yanalinda afya dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababisha na kuwepo kwa lehemu.

JATU imejenga kiwanda cha kukoboa mpunga na kuzalisha mchele katika kata ya Igima maarufu kama Mbingu,kituo hichi kampuni inazalisha mchele na kufungasha katika mifuko maalumu yenye nembo ya kampuni ya JATU na kuingiza sokoni.

JATU imejenga kiwanda cha kusafisha na kuzalisha maharage katika kata ya kibirashi Kijiji cha kwa maligwa.Kupitia kituo hichi kampuni inazalisha maharage na kufungasha katika mifuko maalumu yenye nembo ya kampuni ya JATU na kuingiza sokoni.

Hata hivyo, kampuni ya Jatu imedhamiria kujenga viwanda vingi kadri iwezekanavyo hapa nchini kila wilaya tutakapowekeza kwenye kilimo lazima tuwe na kiwanda maalaum cha kuchakata mazao husika yatakayolimwa katika mradi husika, na katika kutekeleza hili tayari kampuni ya JATU imeanza kujenga kiwanda cha kuchakata ndizi katika wilaya ya Tarime mkoa wa Mara.

Kampuni ya Jatu kupitia viwanda vyake hivyo imekuwa ikijivunia ubora wa bidhaa nzuri

Funga menu
English
Kiswahili English