FUNGA MWAKA 2018 KWA KUNUNUA HISA ZA JATU KWA BEI NAFUU

 

Na; Mwandishi Wetu

Katika kuelekea kukamirisha mwaka 2018 kampuni ya Umma ya Jatu imeamua kupunguza gharama za ununuzi wa hisa kwa wanachama wake na Watanzania kwa ujumla ili kuwapa nafasi watu wengi zaidi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Akifafanua kuhusu punguzo hilo la bei za hisa, Afisa Utawala wa Jatu, Bi Esther Philemon amesema kuwa, punguzo hilo limegawanywa katika makundi mawili yaani wanachama ambao tayari ni wamiliki wa hisa za kampuni na wale ambao bado sio wanahisa.

Bi; Esther amesema kuwa, kundi la kwanza la wanachama ambao tayari ni wanahisa wa Jatu, wao kupitia punguzo hili wataweza kujipatia hisa kumi (10) kwa kiasi cha Shilingi 15,000/= badala ya shilingi 25,000/= bei ya awali au ya kawaida, huku kundi la pili ambao linajumuisha wale wanachama ambao hawakuwahi kabisa kumiliki hisa za Jatu, wao kupitia punguzo hili watakuwa wakipata hisa tano (5) kwa shilingi 10,000/= badala ya shilingi 12,500/= bei ya awali au ya kawaida.

Pamoja na hayo, Bi; Esther amewataka wanachama wote na watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa hii ya punguzo la bei la hisa mwisho huu wa mwaka, kwani ni punguzo la muda tu na linatarajiwa kuhitimishwa ifikapo Desemba 10, 2018, huku akisema kuwa, mbali na magawio ya kila mwaka kutokana na hisa zinazowekezwa na wanachama pia hisa hizo hutumika kama kigezo cha kuweza kushiriki miradi mbalimbali inayopatikana kwenye kampuni.

Ikumbukwe kuwa, kampuni ya Jatu imesajiliwa kama kampuni ya umma na inajishughulisha na biashara ya chakula , viwanda pamoja na masoko hivyo unapowekeza Jatu unakuwa na uhakika wa kupata gawio lako la faida kila misho wa mwaka kulingana na kiasi cha hisa ulichowekeza ndani ya kampuni.

2 replies
  1. Abson
    Abson says:

    Kwenye upande wa fomu ya usajili online inasumbua sana hasa kipengere cha kata(ward), ujumbe inasema no result found au ward id verification

    Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>