KILIMO CHA ALIZETI

 

Jatu ni kampuni ya umma ambayo imejikita katika kilimo, viwanda na masoko. Jatu inatoa fursa kwa wanachama ambao hawakupata nafasi ya kununua mashamba ya kulima Alizeti huko kiteto, kukodi kwa ajili ya msimu wa pili 2018/2019.

Gharama za kukodi mashamba ni kama ifuatavyo; -

Kiteto: kukodi ekari moja ni Tsh. 35,000/= na gharama za kilimo ni Tsh. 211,920/= pamoja na Tsh. 50,000/= ya usimamizi kwa kila ekari. Kwa maelezo zaidi fika ofisi ya jatu iliyo karibu nawe au piga simu namba +255 (0) 762 666 036.

Kwa wanachama wanaolima na Jatu wanaweza kupata mkopo wa kilimo usio na riba kutoka Jatu Saccos. Kwa maelezo zaidi kuhusu Jatu saccos piga simu namba +255 (0) 765 002 660.

 

Zingatia:

Fursa hii ni hadi tarehe 05 Disemba, 2018.                                                                                                                                                                                                                                                   

 

 

“JATU Kilimo, Kilimo ndio msingi wa Jatu”

 

 

 

Imetolewa na;

Moses Lukoo William

Afisa Habari na Mawasiliano, JATU

Dar es salaam.

27 Novemba 2018

FUNGA MWAKA 2018 KWA KUNUNUA HISA ZA JATU KWA BEI NAFUU

 

Na; Mwandishi Wetu

Katika kuelekea kukamirisha mwaka 2018 kampuni ya Umma ya Jatu imeamua kupunguza gharama za ununuzi wa hisa kwa wanachama wake na Watanzania kwa ujumla ili kuwapa nafasi watu wengi zaidi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Akifafanua kuhusu punguzo hilo la bei za hisa, Afisa Utawala wa Jatu, Bi Esther Philemon amesema kuwa, punguzo hilo limegawanywa katika makundi mawili yaani wanachama ambao tayari ni wamiliki wa hisa za kampuni na wale ambao bado sio wanahisa.

Bi; Esther amesema kuwa, kundi la kwanza la wanachama ambao tayari ni wanahisa wa Jatu, wao kupitia punguzo hili wataweza kujipatia hisa kumi (10) kwa kiasi cha Shilingi 15,000/= badala ya shilingi 25,000/= bei ya awali au ya kawaida, huku kundi la pili ambao linajumuisha wale wanachama ambao hawakuwahi kabisa kumiliki hisa za Jatu, wao kupitia punguzo hili watakuwa wakipata hisa tano (5) kwa shilingi 10,000/= badala ya shilingi 12,500/= bei ya awali au ya kawaida.

Pamoja na hayo, Bi; Esther amewataka wanachama wote na watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa hii ya punguzo la bei la hisa mwisho huu wa mwaka, kwani ni punguzo la muda tu na linatarajiwa kuhitimishwa ifikapo Desemba 10, 2018, huku akisema kuwa, mbali na magawio ya kila mwaka kutokana na hisa zinazowekezwa na wanachama pia hisa hizo hutumika kama kigezo cha kuweza kushiriki miradi mbalimbali inayopatikana kwenye kampuni.

Ikumbukwe kuwa, kampuni ya Jatu imesajiliwa kama kampuni ya umma na inajishughulisha na biashara ya chakula , viwanda pamoja na masoko hivyo unapowekeza Jatu unakuwa na uhakika wa kupata gawio lako la faida kila misho wa mwaka kulingana na kiasi cha hisa ulichowekeza ndani ya kampuni.

WAZIRI MWIJAGE AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTOOGOPA KUZALISHA BIDHAA

Na: Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh, Charles Mwijage amewataka wajasiriamali kutokuwa na hofu katika biashara na badala yake kuhakikisha wanazalisha bidhaa za kutosha.

Hayo ameyasema mapema leo tarehe 18.10.2018 wakati alipokuwa kwenye banda la Jatu Plc ndani ya maonesho ya mwanamke mjasiriamali yanayofanyika mkoani Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere Square, ambapo alisema kuwa bidhaa za chakula ni bidhaa ambazo zinatumika kila siku hivyo hakuna haja ya kuhofia kuzalisha bidhaa hizo za kutosha kwani mara nyingi soko lake si la kusuasua.

Read more

WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AWATAKA VIJANA KUIGA MFANO WA JATU PLC

Na: Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu Mstaafu Mh, Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa ipo haja ya vijana kubadili mitazamo yao kuhusu ajira na badala yake wawaze kujiajiri zaidi kama walivyofanya vijana wa kampuni ya Jatu.

Hayo ameyasema leo tarehe 17.10.2018 wakati alipotembelea banda la Jatu Plc ndani ya Maonesho ya Mwanamke Mjasiriamali yanayofanyika mjini Dodoma kwenye Viwanja vya Nyerere Square, ambapo alisema kuwa “inafurahisha kuona vijana kama hawa jatu walivyoamua kujiajiri badala ya kukaa na kusubiri kuajiriwa’ huku akiwasihi vijana wengine kuiga wengine mfano huo.

Read more

JATU PLC: WAKAZI WA TANGA SIKU MOJA INAWEZA KUWATOA KIMAISHA


Na. Mwandishi Wetu
Wakazi wa mkoa wa Tanga wamehaswa kuitumia vyema siku moja ya kesho ya maonesho ya maadhimisho ya wiki ya vijana kufika katika banda la Jatu Plc, kwani wanaweza kupata fursa ambazo zinaweza kuwatoa na kuwafanikisha kimaisha.

Hayo yamesemwa leo tarehe 13.10.2018 na Mkurugenzi wa Jatu Plc, ndugu Peter Isare, akiwa mkoani humo kwenye Viwanja vya Tangamano yanapofanyika maonesho hayo, ambapo alisema kuwa, ni kweli maonesho yanaelekea ukingoni, lakini kwa wale ambao hawajafika bado wanaweza kuitumia siku moja ya kesho iliyobakia kutembelea banda letu na inaweza kuwa moja ya njia yao ya kutoka kimaisha kupitia fursa zetu JATU.

Aidha, Isare alisema kuwa, anashukuru kwa maonesho hayo kwani kila mwanatanga aliyeweza kufika kwenye banda la Jatu amekuwa akioneshwa kufurahishwa na huduma zetu pamoja na fursa tulizonazo na wengi wao wamekuwa wakituambia kuwa fursa za Jatu zinagusa maisha ya Mtanzania ya kila siku, jambo ambalo limekuwa likizidi kutupatia faraja na nguvu mpya zaidi hususani kuelekea ‘Vision 2022.’

Read more

JATU PLC: WAKAZI WA TANGA ZITUMIENI FURSA ZETU ZIWE DARAJA KWENU


Na: Mwandishi Wetu

Wakazi wa mkoa wa Tanga wametakiwa kuzitumia vizuri fursa za Jatu ili kuweza kujikwamua na hali ya umasikini kupitia chakula wanachokula pamoja na mawazo yao ya ubunifu wa bidhaa.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko wa Jatu Plc; Bi Mary Chulle akiwa katika Viwanja vya Tangamano mkoani Tanga yanapofanyika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya vijana, ambapo aliwataka wakazi wa mkoa huo kutembelea banda la Jatu ili kuzifahamu fursa mbalimbali za kampuni hiyo na kuzitumia kama daraja la kuwavusha kuelekea kwenye mafanikio yao kimaisha kupitia ununuzi wa bidhaa na baadaye kulipwa magawio ya faida kila mwezi.

Aidha, Bi; Mary alisema kuwa, wakazi wa mkoa huo wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wanapaswa kuyatumia vyema maonesho hayo kwa kuhakikisha wanafika katika banda la Jatu lililopo upande wa Kaskazini mwa uwanja wa Tangamano karibu na mti mkubwa, ambapo hapo wataelezwa namna wanavyoweza kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao mbalimbali hususani zile za chakula na usafi.

Read more

JATU PLC MWANZA: LENGO LETU NI KUMGUSA KILA MTANZANIA IFIKAPO 2022

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa za chakula na usafi kupitia mfumo wa kisasa wa kimtandao, imesema kuwa ifikapo mwaka 2022 itakuwa imemgusa kila mtanzania wakiwemo wale wa kipato cha chini na cha kati na kuhakikisha wanatokomeza umasikini kupitia chakula wanachokula.

Hayo yamesemwa hivi karibuni (tarehe 02.10.2018) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo; Ndugu; Peter Isare wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa jiji la Mwanza, ambapo amesema kuwa, lengo la Jatu ni kuhakikisha watanzania wanajenga afya na kutokomeza umasikini kupitia chakula wanachokula, hivyo kuna kila sababu ya ifikapo mwaka 2022 watanzania watakao kuwa wamejiunga na Jatu na kuweka juhudi katika fursa zake wawe wamefikia malengo yao kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokomeza umasikini kupitia magawio ya faida watakayolipwa kila mwezi kutokana na chakula wanachonunua kupitia mfumo wa Jatu.

Katika kufikia mafanikio hayo, Isare aliwaeleza wakazi hao wa Mwanza kuwa, kampuni kwa kushirikiana na mabalozi wa bidhaa mbalimbali itahakikisha bidhaa zote muhimu zinapatikana kwa wingi, uhakika na ubora, huku zikiwalenga pia wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwa kuzingatia ujazo wa bidhaa pamoja na bei kulingana na uhalisia wa mkoa au eneo husika.

Read more

JATU PLC: TUTAKUJA KUWA NA SOKO MAALUM LENYE BIDHAA ZA CHAKULA NA USAFI

 

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc imesema kuwa inampango wa kuanzisha soko maalum la bidhaa zake pamoja na zile za mabalozi wa kampuni hiyo ili kuwahakikishia wanachama wake upatikanaji wa urahisi na uhakika wa bidhaa hizo ili Watanzania wajenge afya na kutokomeza umasikini kwa uhakika zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ndugu; Peter Isare wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Musoma mkoani Mara hivi karibuni, ambapo alisema kuwa, mpango huo wa kuanzisha soko hilo maalum utasaidia kufikiwa kwa urahisi dira ya Jatu ya mwaka 2022 maarufu kama ‘Vision 2022’.

Aidha, Isare alisema kuwa, siku zote Jatu imekuwa ikijipambanua kama kampuni yenye kuenenda na ubunifu zaidi na kuzichua changamoto kuwa fursa, hivyo anaamini kuwa hata suala hilo la kuanzisha soko hilo linaweza kuwa ni kama ndoto lakini ni jambo ambalo linawezekana kabisa endapo misingi ya Jatu ikizingitiwa ambayo ni Umoja, Ubunifu, Uthubutu, Bidii na Huduma bora.

Read more

JATU PLC: Kutoa elimu mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji, kuhusu kula kwa faida

Na:Mwandishi Wetu

Katika kuhakikisha Watanzania wote wanafikiwa na huduma pamoja na fursa zote zinazotolewa na kampuni ya Jatu Plc, kampuni hiyo kupitia idara yake ya masoko imeamua kutembea kijiji kwa kijiji ili kuwafikia watanzania waliopo katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza mapema jana (September 15,2019) baada ya kutembelea mkoani Lindi katika vijiji vya Kilangala A na B, Afisa Masoko wa Jatu; Bi; Mary Chulle amesema kuwa, lengo la kuendesha zoezi hilo la mtaa kwa mtaa pamoja na kijiji kwa kijiji ni kutaka kukutana na watanzania wenye nia ya dhati ya kujenga afya na kutokomeza umasikini kupitia matumizi ya chakula wanachokula kila siku.

Read more