TAARIFA KWA UMMA

Kampuni ya JATU (JATU PLC) inatoa taarifa kwa umma kuwa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (“CMSA”), katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania) tarehe 31 Mei 2021 iliidhinisha waraka wa matarajio wa Kampuni ya JATU PLC kwa ajii ya kuuza kwa umma, katika soko la awali, hisa 15,000,000 kwa bei ya Sh. 500 kwa kila hisa.

Hisa hizo zinauzwa kuanzia tarehe 1 Juni 2021 mpaka tarehe 15 Julai 2021 na zitaorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) tarehe 29 Julai 2021. Katika kipindi cha mauzo ya hisa hizo katika soko la awali, uuzaji wa hisa za JATU PLC kwenye soko la upili (DSE) utasimama hadi tarehe 28 Julai 2021 siku moja (1) kabla ya kuorodheshwa kwa hisa mpya. Kwa mantiki hiyo, uuzaji wa hisa za JATU PLC katika DSE utaendelea kuanzia tarehe 29 Julai 2021 baada ya kuorodheshwa kwa hisa mpya za JATU PLC.

Waraka wa matarajio wa JATU PLC unapatikana katika tovuti ya kampuni htps//www.jatu.co.tz na kwa washauri wa uwekezaji na watendaji wa Soko la Hisa (brokers/dealers) walioidhinishwa na CMSA. Hisa hizi zinauzwa kwa wawekezaji wa Tanzania na wa nje ya Tanzania; wenye rika na jinsia zote, ikiwa ni pamoja na wanawake, wanaume, watoto, vijana na watu wazima; watu wenye ulemavu; waishio mijini na vijijini. 

Kwa maelezo zaidi kuhusu hisa za JATU Plc, wasiliana na washauri wa uwekezaji; watendaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam na mawakala wa mauzo walioidhinishwa na CMSA.

FOMU YA MAOMBI YA KUNUNUA HISA ZA JATU PLC

Unaweza kununua HISA kwa kupakua fomu hapo chini kisha jaza taarifa zako na utume kwenda kwenda kwenye email hisa@jatu.co.tz.

Pakua fomu ya kiswahili hapa:

Pakua fomu ya kingereza hapa:

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili