JATU PLC: ILIVYOJIPANGA KUBORESHA KILIMO CHA MPUNGA.

Kampuni ya Jatu Plc  tarehe 14/7/2018, imekutana na wakulima pamoja na wajasiriamali wa Wilaya ya Kilombero na kuzungumza kuhusu uboreshaji wa kilimo cha Mpunga.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero uliopo ifakara mjini eneo la Kibaoni, Mkurugenzi wa Jatu PLC, ndugu Peter Isare alisema kuwa, dhamira ya kampuni ni kuhakikisha kilimo cha zao la mpunga kinaimarika na kuwa kilimo chenye tija kwa wakulima kwa kulima kisasa na kupata mavuno mengi zaidi.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Isare aliambatana na Meneja wa Jatu tawi la Mbingu, ndugu, Paul Kapalata ambaye hivi karibuni ametokea nchini Ufilipino kupata mafunzo ya kilimo cha mpunga, ambapo Isare alisema kuwa, kampuni itawatumia wataalam wake hao kuhakikisha kilimo hicho kina kuwa bora.

Aidha, Isare kupitia kikao hicho aliwaeleza wakulima na wajasiriamali kuhusu umuhimu wa kuwekeza Jatu kwa kununua hisa na hivyo kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni.

Mbali na hayo, Isare ameendelea kuwahimiza wanachi wa Kilombero na maeneo jirani wakiwemo wakulima na wafanyabiashara kujiunga na Jatu ili kupata soko la uhakika la bidhaa zao za kilimo na bidhaa nyingine za chakula na usafi ndani ya Jatu Plc.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo amesema kuwa kampuni itaendelea kutoa elimu za mara kwa mara kuhusu kilimo , viwanda, na masoko ikiwa ni moja ya kutimiza kampeni ya kuelekea dira ya mwaka 2022, kampeni ambayo lengo lake ni kutengeneza mabilionea wa kudumu wasiopungua 50.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>