JATU PLC: Kutoa elimu mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji, kuhusu kula kwa faida

Na:Mwandishi Wetu

Katika kuhakikisha Watanzania wote wanafikiwa na huduma pamoja na fursa zote zinazotolewa na kampuni ya Jatu Plc, kampuni hiyo kupitia idara yake ya masoko imeamua kutembea kijiji kwa kijiji ili kuwafikia watanzania waliopo katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza mapema jana (September 15,2019) baada ya kutembelea mkoani Lindi katika vijiji vya Kilangala A na B, Afisa Masoko wa Jatu; Bi; Mary Chulle amesema kuwa, lengo la kuendesha zoezi hilo la mtaa kwa mtaa pamoja na kijiji kwa kijiji ni kutaka kukutana na watanzania wenye nia ya dhati ya kujenga afya na kutokomeza umasikini kupitia matumizi ya chakula wanachokula kila siku.

Aidha, Bi; Mary amesema kuwa dhamira ya Jatu ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ambaye amejiunga na Jatu anaishi kwa kula kwa faida kama mfumo wa masoko wa Jatu Plc unavyoelekeza.

Mbali na hayo, Afisa masoko huyo amewataka viongozi wa mitaa na vijiji ambao watapenda kufikiwa katika maeneo yao na kupewa elimu kuhusu kula kwa faida ndani ya JATU basi wasisite kuwasiliana na timu ya masoko ili waweze kulifanikisha hilo na kutokomeza umasikini.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>