JATU PLC MWANZA: LENGO LETU NI KUMGUSA KILA MTANZANIA IFIKAPO 2022

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc inayojishughulisha na uuzaji wa bidhaa za chakula na usafi kupitia mfumo wa kisasa wa kimtandao, imesema kuwa ifikapo mwaka 2022 itakuwa imemgusa kila mtanzania wakiwemo wale wa kipato cha chini na cha kati na kuhakikisha wanatokomeza umasikini kupitia chakula wanachokula.

Hayo yamesemwa hivi karibuni (tarehe 02.10.2018) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo; Ndugu; Peter Isare wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa jiji la Mwanza, ambapo amesema kuwa, lengo la Jatu ni kuhakikisha watanzania wanajenga afya na kutokomeza umasikini kupitia chakula wanachokula, hivyo kuna kila sababu ya ifikapo mwaka 2022 watanzania watakao kuwa wamejiunga na Jatu na kuweka juhudi katika fursa zake wawe wamefikia malengo yao kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokomeza umasikini kupitia magawio ya faida watakayolipwa kila mwezi kutokana na chakula wanachonunua kupitia mfumo wa Jatu.

Katika kufikia mafanikio hayo, Isare aliwaeleza wakazi hao wa Mwanza kuwa, kampuni kwa kushirikiana na mabalozi wa bidhaa mbalimbali itahakikisha bidhaa zote muhimu zinapatikana kwa wingi, uhakika na ubora, huku zikiwalenga pia wananchi wa kipato cha chini na cha kati kwa kuzingatia ujazo wa bidhaa pamoja na bei kulingana na uhalisia wa mkoa au eneo husika.

Aidha, Isare aliwataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kujiunga na Jatu na wale wenye bidhaa mbalimbali za chakula na usafi waziwasilishe katika ofisi za Jatu Mwanza zilizopo Barabara ya Nkurumah Mkabala na Ndija Photo Studio Plot no 37 ndani ya Wilaya ya Nyamagana ili kupata soko la uhakika kupitia mfumo wa Jatu (J.shop).

Naye Meneja wa Jatu Kanda ya ziwa ndugu; Ampelius Rweyemamu, hakusita kutoa tathimini yake ndogo kuhusu kampeni ya kuelekea dira ya mwaka 2022 maarufu kama ‘Vision 2022’ inayoendeshwa nchi nzima na kampuni hiyo na kusema kwamba, “Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo mkoa wa Mwanza umeonekana bado uko nyuma katika kuchangamkia fursa za Jatu kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya watu kutoelewa ipasavyo dhamira ya JATU na hivyo kituo changu cha mwanza kimedhamiria kuziondoa changamoto hizo kwa kuanzisha utaratibu wa kuwafikia wakazi wa jiji hilo popote walipo (mtaa kwa mtaa) na kuhakikisha wanaielewa Jatu na kuanza kuzitumia ipasavyo fursa zote zinazotolewa na kampuni hiyo”.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>