JATU PLC: SAFARI YA DSE YAPAMBAMBA MOTO

Na: Mwandishi Wetu
KUELEKEA soko la hisa (DSE) kampuni ya Jatu imeamua kuanzisha kampeni rasmi mwezi huu wa tano ya kuwahamasisha wanahisa wa Jatu kuwakaribisha wanahisa wapya ambao watakuwa tayari kununua hisa za kampuni hiyo pindi itakapoingia soko la hisa la DSE.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Jatu, Ndugu Peter Isare, kupitia taarifa yake iliyotolewa Mei, 01, 2019, ambapo alieleza kuwa, kampeni hiyo itafanyika kupitia magroup maalum ya mtandao wa kijamii wa Whatsapp, ambayo yatakuwa yakihusisha watu wote wenye uwezo wa kununua hisa angalau zenye thamani ya Laki Moja na Elfu Ishirini na Tano (125,000/=), na kupitia magroup hayo semina mbalimbali kuhusu elimu ya hisa kwa ujumla zitakuwa zikitolewa kupitia wataalam maalum wa Jatu.

Aidha, Isare kupitia taarifa hiyo aliwataka wanajatu ambao wanatamani kuiona jatu inafanikisha mpango huo kujitokeze na kuunga mkono kwa kuunda magroup ya Whatsapp yenye watu 250 na kuyawasilisha Jatu ili yaweze kuingia kwenye semina elekezi ya hisa za Jatu, ambapo watakuwa wakielekezwa namna ya kunufaika kutokana na kufanya manunuzi ya hisa za Jatu, hali ambayo itachangia watu wengi kuielewa kampuni na kujiandaa kununua hisa pindi milango itakapofunguliwa.

Pamoja na hayo, Isare amesema kuwa, ili kuifanya kampeni hii kuwa na kasi zaidi kampuni itakuwa ikitoa zawadi nono kwa wale watakaofanikisha zoezi hili (kuunda magroup ya Whatsapp yenye watu 250) na hivyo kuwataka wanachama kuichukulia kampeni hii kama fursa ya kipato kwao.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>