JATU PLC: TUTAKUJA KUWA NA SOKO MAALUM LENYE BIDHAA ZA CHAKULA NA USAFI

 

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc imesema kuwa inampango wa kuanzisha soko maalum la bidhaa zake pamoja na zile za mabalozi wa kampuni hiyo ili kuwahakikishia wanachama wake upatikanaji wa urahisi na uhakika wa bidhaa hizo ili Watanzania wajenge afya na kutokomeza umasikini kwa uhakika zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Ndugu; Peter Isare wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Musoma mkoani Mara hivi karibuni, ambapo alisema kuwa, mpango huo wa kuanzisha soko hilo maalum utasaidia kufikiwa kwa urahisi dira ya Jatu ya mwaka 2022 maarufu kama ‘Vision 2022’.

Aidha, Isare alisema kuwa, siku zote Jatu imekuwa ikijipambanua kama kampuni yenye kuenenda na ubunifu zaidi na kuzichua changamoto kuwa fursa, hivyo anaamini kuwa hata suala hilo la kuanzisha soko hilo linaweza kuwa ni kama ndoto lakini ni jambo ambalo linawezekana kabisa endapo misingi ya Jatu ikizingitiwa ambayo ni Umoja, Ubunifu, Uthubutu, Bidii na Huduma bora.

Isare aliongeza kuwa, matarajio ya soko hilo maalum ni kuwa lenye kusheheni bidhaa za chakula na zile za usafi na kuwaruhusu wanachama wake kuuza na kununua bidhaa kwa msaada wa mawakala na kisha baadaye kupata magawio yao ya kila mwezi kutokana na manunuzi yao.

Naye Meneja wa Jatu kanda ya ziwa, ndugu: Ampelius Rweyemamu aliwataa wakazi wote wa kanda ya ziwa na maeneo jirani kujiunga na Jatu na kuanza kutumia huduma zake ili kuweza kujenga afya zao kutokana na matumizi ya bidhaa hizo pamoja na kujitengenezea kipato.

Itakumbukwa kwamba kwasasa Jatu Plc inaendelea na semina zake katika miko ya kanda ya ziwa na leo (02.10.2018) itakuwa ni zamu ya kuzungumza na wakazi wa Mwanza na maeneo jirani kuhusu fursa zinazopatikana ndani ya Jatu.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>