JATU PLC: WAKAZI WA TANGA SIKU MOJA INAWEZA KUWATOA KIMAISHA


Na. Mwandishi Wetu
Wakazi wa mkoa wa Tanga wamehaswa kuitumia vyema siku moja ya kesho ya maonesho ya maadhimisho ya wiki ya vijana kufika katika banda la Jatu Plc, kwani wanaweza kupata fursa ambazo zinaweza kuwatoa na kuwafanikisha kimaisha.

Hayo yamesemwa leo tarehe 13.10.2018 na Mkurugenzi wa Jatu Plc, ndugu Peter Isare, akiwa mkoani humo kwenye Viwanja vya Tangamano yanapofanyika maonesho hayo, ambapo alisema kuwa, ni kweli maonesho yanaelekea ukingoni, lakini kwa wale ambao hawajafika bado wanaweza kuitumia siku moja ya kesho iliyobakia kutembelea banda letu na inaweza kuwa moja ya njia yao ya kutoka kimaisha kupitia fursa zetu JATU.

Aidha, Isare alisema kuwa, anashukuru kwa maonesho hayo kwani kila mwanatanga aliyeweza kufika kwenye banda la Jatu amekuwa akioneshwa kufurahishwa na huduma zetu pamoja na fursa tulizonazo na wengi wao wamekuwa wakituambia kuwa fursa za Jatu zinagusa maisha ya Mtanzania ya kila siku, jambo ambalo limekuwa likizidi kutupatia faraja na nguvu mpya zaidi hususani kuelekea ‘Vision 2022.’

Pamoja na hayo, Isare aliongeza kwa kusema kuwa, wakazi wa Tanga ni lazima watambue kuwa, fursa kama hizo ni nadra kutokea mara kwa mara hivyo ni vyema wakazi wa mkoa huo wakaitumia siku moja iliyobakia kabla ya kuhitimisha maonesho hayo kufika katika viwanja vya Tangamano na kutembelea banda la Jatu Plc lililopo upande wa Kaskazini mwa uwanja huo karibu na mti mkubwa, ambapo hapo mbali na kuelezwa kuhusu kula kwa faida pia wataelezwa namna wanavyoweza kujitengenezea soko la uhakika la bidhaa mbalimbali hususani zile za chakula na usafi.

Naye , Afisa Mkuu wa Masoko wa Jatu Plc, Bi; Mary Chulle yeye aliwasihi wakazi wa mkoa huo wa Tanga hususani wajasiriamali na wafanyabiashara kuitumia vyema siku moja ya maonesho hayo iliyobakia kwa kuhakikisha wanafika katika banda la Jatu ili kupata nafasi ya kufahamu namna watakavyoweza kunufaika na Jatu kwa kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao mbalimbali, huku wateja wao ambao ni wanachama nao wakinufaika kwa kutokomeza umasikini kupitia kulipwa magawio ya faida kutokana na manunuzi yao.

Ikumbukwe kwamba maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 08.10.2018 na yatahitimishwa kesho tarehe 14.10.2018. huku yakiongozwa na kauli mbiu isimayo “ Mazingira salama kwa vijana”

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>