JATU PLC: WAKAZI WA TANGA ZITUMIENI FURSA ZETU ZIWE DARAJA KWENU


Na: Mwandishi Wetu

Wakazi wa mkoa wa Tanga wametakiwa kuzitumia vizuri fursa za Jatu ili kuweza kujikwamua na hali ya umasikini kupitia chakula wanachokula pamoja na mawazo yao ya ubunifu wa bidhaa.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko wa Jatu Plc; Bi Mary Chulle akiwa katika Viwanja vya Tangamano mkoani Tanga yanapofanyika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya vijana, ambapo aliwataka wakazi wa mkoa huo kutembelea banda la Jatu ili kuzifahamu fursa mbalimbali za kampuni hiyo na kuzitumia kama daraja la kuwavusha kuelekea kwenye mafanikio yao kimaisha kupitia ununuzi wa bidhaa na baadaye kulipwa magawio ya faida kila mwezi.

Aidha, Bi; Mary alisema kuwa, wakazi wa mkoa huo wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara wanapaswa kuyatumia vyema maonesho hayo kwa kuhakikisha wanafika katika banda la Jatu lililopo upande wa Kaskazini mwa uwanja wa Tangamano karibu na mti mkubwa, ambapo hapo wataelezwa namna wanavyoweza kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao mbalimbali hususani zile za chakula na usafi.

Mbali na hayo, Bi; Mary aliongeza kuwa, Jatu ni kampuni ambayo imelenga kujenga afya na kutokomeza umaskini, hivyo kila Mtanzania akiwemo mkazi wa Tanga hana budi kujiunga na kampuni hii ili kujenga afya yake kupitia bidhaa za vyakula zinazoandaliwa na kampuni pamoja na zile za mabalozi wake na kuuzwa kupitia mfumo wa masoko ya Jatu na mwishowe kila mwanachama hulipwa gawio la faida kutokana na manunuzi yake.

Ikumbukwe kwamba maonesho hayo yameanza rasmi tarehe 08.10.2018 na yatahitimishwa tarehe 14.10.2018. huku yakiongozwa na kauli mbiu isimayo “ Mazingira salama kwa vijana”

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>