JATU PLC: YAELEZA KUHUSU MAVUNO YA MAHINDI KITETO

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc tarehe 04/08/2018, imekutana na wanahisa wa kampuni hiyo na kuzungumzia agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na matokeo ya kilimo kwa mwaka 2017 – 2018 kuelekea soko la hisa DSE na gawio la hisa kwa mwaka 2017.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Maonesho Sabasaba, barabara ya Kilwa zilizopo ofisi kuu za kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Jatu PLC, ndugu; Peter Isare alisema kuwa, awamu ya kwanza ya kilimo kwa mwaka 2017 -2018 imekamilika na sasa tayari zoezi la uvunaji linaendelea na wapo katika hatua za mwisho za kumalizia uvunaji wa mahindi kabla ya kuhamia kwenye uvunaji wa alizeti.
Aidha, Isare amesema kuwa, kila ekari moja ya mahindi imetoa wastani wa gunia 11, ambapo hiyo ni asilimia 40% ya kilimo cha mahindi , huku asilimia 60% zinazobaki zikiwa ni alizeti.

Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo la mavuno ya mahindi ya Kiteto – Manyara, Isare amewataka wakulima walioshiriki kilimo kwa mwaka 2017 -2018 kuanza kufika ofisini ili kufanya utaratibu wa malipo yao kwani kwasasa wanapokea maombi hayo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kila siku za wiki.

Hata hivyo, Isare aliwaeleza wakulima hao kuwa lengo la kufika ofisini kwasasa ni kwaajili ya kufanya mchanganuo na uhakiki wa taarifa zao kwa kushirikiana na mhasibu kabla ya malipo kuanza kufanyika mara moja.

Kuhusu gawio la hisa, Isare alisema kuwa wanahisa nao wanaruhusiwa kufika ofisini ili kupata utaratibu mzuri wa kupata magawio yao yatokanayo na hisa zao, ambapo hadi sasa tayari mchakato umeshaanza ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi zaidi.

Mbali na hayo Mkurugenzi huyo alisisitizia suala la kampuni kuelekea katika Soko la Hisa na kusema kuwa, hadi sasa wataalamu ambao wanasimamia na kufuatilia suala hilo wanaendelea vyema na kazi hiyo, huku wakitarajia kuwa ifikapo mwezi Novemba mwaka huu kampuni itakuwa tayari imeingia kwenye soko la hisa DSE jambo ambalo litachangia kampuni kukua zaidi na kuwekeza zaidi katika kilimo cha kisasa pamoja na viwanda, hivyo kila mmoja anapaswa kuwashirikisha ndugu jamaa pamoja na marafiki ili kununua hisa kadri wawezavyo kuanzia sasa na pindi tutakapoingia soko la hisa.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>