JATU PLC: YAENDELEA KUWAFUNGUA WATANZANIA KUHUSU BIASHARA YA CHAKULA SABASABA

Na: Mwandishi Wetu

Ikiwa leo ni tarehe 08.07.2018 Kampuni ya Jatu Plc imeendelea kutoa fursa kwa moyo mkunjufu kwa wananchi wanaotembelea maonyesho hayo ya 42 ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendela jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika maonyesho hayo mapema leo, Meneja Rasilimali watu wa Jatu Bi; Esther Kiuya amesema kuwa, kinachofanyika hivi sasa ni kubadili mitizamo ya Watanzania wenzetu na kuwafanya kuanza kuamini kwamba chakula wanachokula kinaweza kuwa biashara na kuwaingizia kipato.

Aidha, Bi; Kiuya amesema kuwa, waliotembelea banda la Jatu wamekuwa wakifurahishwa na huduma za kampuni, huku wajasiriamali wakisema kuwa Jatu ikitumika vizuri inaweza kuwa daraja la mafanikio kwa wajasiriamali wa bidhaa za chakula na usafi pamoja na kilimo bora.

Mbali na hayo, Bi; Kiuya amesema kwamba banda la jatu limekuwa likitembelewa na wananchi wengi, lakini pia tumetembelewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Faustine Ndungulile ambaye naye alipata kuelezwa kwa kina kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni ya Jatu.

Pamoja na hayo, Bi; Kiuya ameendelea kuwasihi wananchi ambao bado hawajatembelea maonyesho hayo pindi watakapotembelea wasiache kufika katika banda la Jatu ili wajiunge na Jatu na kunufaika na fursa lukuki zinazoendelea ndani ya Jatu ikiwa ni pamoja na kilimo, viwanda, masoko, mikopo pamoja na ununuzi wa hisa.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>