JATU PLC: YAWAFUATA TENA WANAMTWARA KUTOA SEMINA

Na: Mwandishi Wetu

Kampuni ya Jatu Plc, leo tarehe 05.05.2018 ilikuwa mkoani Mtwara ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya dira ya mwaka 2022 maarufu kama ‘Vision 2022’.
Akizungumza na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha JATU, Afisa Masoko wa Jatu Plc, Bi; Mary Chulle, amesema kwamba, semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa ALPHA uliopo mkoani Mtwara mtaa wa LIGULA karibu na JIONEE kuanzia saa 04:00 asubuhi.

Aidha, Bi; Mary amesema kwamba, lengo la semina hiyo mkoani Mtwara ni kutaka kujua maendeleo ya wanachama na mawakala wa kampuni hasa kuhusu utekelezaji wa kampeni ya ‘Vision 2022’ .

“Tunachohitaji ni kujua ni kwa namna gani wanachama wetu na mawakala wa Mtwara wameendelea kutekeleza misingi ya kuelekea ‘Vision 2022’ ikiwa ni pamoja na kuendelea kujenga vizazi, mtandao wa watu 10 na kuhakikisha kila mmoja anakula angalau kilo 100 kwa mwezi”, alisema Bi; Mary.

Pia Bi; Mary ameongeza kwa kusema kwamba, “ tumekusudia kuangazia ni kwa namna gani wanamtwara wameendelea kuunda vikundi pamoja na kufikiria mawazo ya ubunifu ambayo yatasaidiwa kuendelezwa na kampuni”.

Naye Afisa Habari wa Jatu Plc, Ndugu, Moses Lukoo , amesema kuwa pamoja na mambo mengine semina hiyo itaenda sambamba na kuangazia namna ya utendaji kazi wa mawakala wa mkoa huo hasa katika mfumo wa Jatu na kuwasaidia pale patakapoonekana bado kunachangamoto.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>