JATU YASHIRIKI MAONESHO YA BIDHAA ZA VIWANDA

Na: Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Jatu Plc ni miongoni kati ya makampuni na mashirika ambayo yanashiriki maonesho ya bidhaa zinazoandaliwa na viwanda vya Tanzania yanayoanza ramsi leo Desemba 05,2019.

Maonesho hayo ambayo yanafanyika katika Viwanja vya Maonesho Sabasaba barabara ya Kilwa, yamelenga kutambua mchango wa viwanda nchini yatahudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na viongozi wa kiserikali, huku ufunguzi rasmi ukitarajiwa kufanyika Desemba 07, 2019 na kuongozwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Mhandisi; Stella Manyanya.

Kupitia maonesho hayo Jatu inawakaribisha wanachama na wasio wanachama kujitokeza katika maonesho hayo muhimu na kutembelea banda letu la Jatu namba 32 ambapo watapokea huduma nzuri kuhusu masuala ya kilimo, viwanda na masoko pamoja na mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kupitia Jatu Sacoss.

Mbali na huduma hizo, Jatu pia imeandaa bidhaa za kutosha ambazo huandaliwa na viwanda vyake ambazo ni pamoja na Unga wa sembe na dona, mafuta ya alizeti, mchele, karanga pamoja na maharagwe.

Itakumbukwa kwamba maonesho hayo yanatarajiwa kufikia kilele Desemba 09.2019.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili