JATU YAWAFIKIA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KWA KISHINDO

Na: Mwandishi Wetu

HATIMAYE Kampuni ya Jatu Plc imefanikiwa kuwafikia wakazi wa jiji la Arusha baada ya jana tarehe 28.07.2018 kufungua ofisi (tawi) jipya jijini humo.

Kufunguliwa kwa ofisi hiyo jijini Arusha ni sehemu ya muendelezo wa kuhakikisha huduma za Jatu zinaenea kwa kasi na kwa kishindo ili kuwafikia Watanzania wote nchi nzima na kuhakikisha Wanajenga Afya na Kutokomeza Umasikini kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo.

Akizungumza katika semina na ufunguzi wa tawi hilo jipya uliofanyika katika Hoteli ya Golden Rose ndani ya ukumbi wa Kitenge uliopo Arusha mjini, Mkurugenzi Mkuu wa Jatu, Ndugu; Peter Isare amesema kwamba, tawi hilo litakuwa likitoa huduma zote za Jatu ikiwa ni pamoja na elimu ya Jatu kwa ujumla pamoja na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani yake ambazo ni Kilimo, Viwanda pamoja na masoko.

Aidha, Isare amesema kuwa, ofisi hiyo pia itakuwa na bidhaa zote zinazoandaliwa na kampuni ya Jatu pamoja na zile za mabalozi, ambapo kila mwanachama atakapokuwa akinunua bidhaa hizo atakuwa akipata gawio lake la faida kila mwisho wa mwezi.

Isare pia ameongeza kwa kusema kuwa, ofisi hiyo itakuwa ikitoa huduma za mikopo kupitia JATU SACCOS (JSL) ambapo wakazi wa jiji la Arusha wenye kukidhi vigezo wataweza kukopeshwa mikopo mbalimbali ikiwemo mikopo ya Kilimo, Elimu na ile ya dharula.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo amewataka wakazi wa jiji la Arusha kuchangamkia fursa ya ununuzi wa hisa za kampuni kabla ya kuelekea katia SOKO LA HISA ili kusaidia ukuaji wa viwanda kwa kasi, lakini pia ili na wao waweze kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni ya jatu kupitia ununuzi wa hisa hizo.

Akifafanua zaidi kuhusu eneo inapopatikana ofisi hiyo ya JATU jijini Arusha, Mkurugenzi Isare, amesema kuwa, ofisi hiyo ipo eneo la KALOLENI jengo la CONDO BUILDINGS ghorofa ya pili na rasmi itaanza kutoa huduma tarehe 01.08.2018.

Ikumbukwe kwamba, kufunguliwa kwa ofisi hii mpya mjini Arusha ni muendelezo wa kuwafikia Watanzania ambapo hadi sasa kampuni imefanikiwa kuwa na ofisi (matawi) mkoani Dodoma, Kibaigwa, Morogoro Kilombero kata ya Igima (Mbingu), Kiteto mkoani Manyara, Mwanza na sasa Arusha, Dar es Salaam- Sabasaba Maonesho, Barabara ya Kilwa (MAKAO MAKUU) , huku mikoa mingine ikiwakirishwa na mawakala wa kampuni katika utoaji wa huduma za JATU.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>