jatu kilimo

Kampuni ya Jatu inaendesha na kusimamia miradi mbalimbali ya kilimo kwa kushirikiana na wanachama wake.

Kilimo kwetu Jatu ndio msingi na nguzo muhimu ya kampuni, ambapo Jatu hutafuta maeneo/mashamba na kuyafanyia utafiti wa kitaalam na kisheria na pindi tunapojiridhisha kwamba maeneo husika ni mazuri kwa kilimo kusudiwa hapo ndipo kampuni huwashirikisha wanachama wake ili waweze kumiliki mashamba hayo. Huku kampuni ikiwahakikishia wanachama wake soko la uhakika la mazao yao kupitia viwanda vyetu.

Mara zote Jatu tumekuwa tukiwashauri wanachama wetu kumiliki mashamba makubwa na yenye rutuba ambayo hukubali mazao ambayo kampuni huyahitaji katika uzalishaji wa bidhaa zetu. Hadi sasa JATU kwa kushirikiana na wanachama wetu tumefanikiwa kumiliki mashamba makubwa matatu yanayopatikana mkoani Manyara, Morogoro na Tanga

Mkoani Manyara wilayani Kiteto Jatu inaendesha mradi wa kilimo cha mahindi na alizeti, ambapo zaidi ya ekari 2000 tayari zimelimwa, huku matarajio yakiwa ni kufikisha ekari 5000 za mazao hayo ifikapo mwaka 2022.

Mkoani Morogoro wilayani Kilombero Jatu imejikita katika kilimo cha mpunga, ambapo hadi kufikia sasa ekari zadi ya 200 zimeshalimwa, huku kampuni ikiendeleza uwekezaji zaidi katika kilimo hicho ili ifikapo mwaka 2022 kuwe na ekeri takribani 1000 zitakazokuwa zimelimwa zao hilo la mpunga.

Aidha, mpango wetu JATU ni kuhakikisha tunaanzisha mashamba kila wilaya hapa nchini Tanzania na mashamba hayo tutayawekea miundombinu ya umwagiliaji, huku yakiambatana na viwanda ndani yake.

kwa kujua kilimo zaidi na maelezo mengine tafadhali bonyeza hapa https://jatukilimo.com/

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili