bidhaa zetu jATU

Jatu tumejikita katika bidhaa za chakula kama vile;-

 1. Nafaka (Mchele, Sembe, Dona, Karanga, Unga wa lishe na Ngano)
 2. Mboga (Maharage, Samaki, Dagaa n.k)
 3. Viungo (Mafuta ya alizeti, Chai Mbadala, Sukari, Chumvi)
 4. Vinywaji (Maji ya kunywa, juisi za matunda)
 5. Matunda (Ndizi, Nanasi, Parachichi)

(Hadi sasa tayari tuna bidhaa zifuatazo; Mchele, unga wa dona, sembe, mafuta ya kupikia ya alizeti, majani ya chai mbadala, chumvi, maji ya kunywa, maharage, karanga, na vingine vitaendelea kuja).

Jatu imejikita na bidhaa ambazo hutumika kila siku katika familia zetu, huku malengo yetu ni kuwa na bidhaa zote muhimu katika JATU APP ifikapo mwaka 2022

kuhusu masoko ndani ya JATU

Masoko ya uuzaji wa bidhaa za Jatu ni ya mfumo wa kimtandao (Network Marketing). 

Biashara ya masoko ya mtandao ni ya kupashana habari kati ya mtu mmoja hadi mwingine kuhusu bidhaa za kampuni.

Faida ambayo hupatikana kwenye biashara ya masoko ya mtandao ya JATU ndiyo hutumika kumtengenezea mwanachama kipato cha kudumu cha kila mwezi kutokana na manunuzi yake pamoja na timu yake.

Mtu anayejiunga na kampuni ya Jatu ni lazima pia akubali kuwa miongoni mwa wanunuzi wa bidhaa zinazoandaliwa na Jatu na ndipo atakuwa akipata sehemu ya faida ya kila bidhaa anayonunua (gawio la faida la kila mwezi)

Soko la biashara ya mtandao huenda sambamba na utengenezaji wa mtandao wa walaji wa bidhaa za jatu. Kila anaponunua mtu aliye katika mtandao wako kuanzia kizazi cha 1 – 5 wewe utakuwa ukipata gawio ambalo ni sawa na asilimia 40% ya faida yote.

Jatu pia imekuwa ikitoa fursa ya masoko ya bidhaa za wajasiriamali wengine (JATU BALOZI) ambao ni wanachama kwa kuruhusu bidhaa zao kuuzwa kupitia mfumo wa Jatu (JATU APP) endapo bidhaa husika itakuwa na ubora na kuhitajika sokoni. (Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi au fika katika ofisi zetu).

Jatu tunatumia mfumo wa masoko ya mtandao (Network Marketing) katika kutoa huduma na manunuzi ya bidhaa za chakula, usafi na nishati.

Biashara ya masoko ya mtandao ni biashara ya kupashana habari kati ya mtu mmoja hadi mwingine kuhusu huduma na bidhaa ambazo hupatikana kupitia mfumo wetu (Jatu Market).

Mfumo wa jatu (Jatu Application) humpatia mwanachama (mteja) nafasi ya kufanya manunuzi ya bidhaa za kila siku kwa kuweka oda kupitia mfumo huo na kisha kufikishiwa hadi sehemu alipo (nyumbani, kazini) pindi mteja anapokamirisha malipo.

Ili kufanikisha kufanya manunuzi au oda kupitia mfumo wa jatu mwanachama anapaswa kufuata taratibu zifuatazo:-

 1.  Kupakua App ya jatu kupitia playstore na kisha kujisajili kwa kujaza taarifa zako sahihi kulingana na maelekezo.
 2.  Ingia katika APP ya Jatu kwa namba yako ya uanachama yenye utambulisho waAA-XXXX au AB-XXXX.
 3. Unapoingia ndani ya APP utaona kuna sehemu imeandikiwa ‘Shop’ hapo ndipo sehemu ya kuweka oda ambapo utakuta alama ya jumlisha na utaibonyeza ili kukuletea orodha ya mikoa yenye bidhaa, kisha chagua mkoa ulipo na utaona bidhaazote  zinazopatikana kwenye mkoa huo husika.
 4.  Baada ya kuona bidhaa hizo ndipo utaweza kufanya uchaguzi wa bidhaa unazotaka na kuweka oda, ukituma oda kabla ya kwenda utaombwa kuchagua wakala unayemfahamu na ukituma utaulizwa eneo ambalo mzigo unapaswa kwenda ili kumrahisishia msafirishaji kujua mzigo unaenda wapi (eneo) na afisa usafirishaji atawasiliana na wewe mteja ili kuanza safari ya kuwasilisha bidhaa zako.
 5.  Oda ikishatumwa utapokea ujumbe mfupi wa maneno (meseji) kupitia simu yako ya mkononi inayotambulika Jatu, ujumbe huo utakuwa ukifanana na huu ”Bill namba AB-2075-SB-0001 yenye kumbukumbu no. 213505 imefanikiwa kutengenezwa Tafadhali lipia jatu Sh. 5000/= ili uweze kuletewa mzigo” ujumbe huo unamuonesha mteja husika kwamba amefanikiwa kuweka oda na anapaswa kulipia kiwango kilichoainishwa kwenye ujumbe husika.
 6. Baada ya ujumbe huo mteja utapaswa kuingia menu ya Tigo Pesa au M-Pesa na ufuate taratatibu zifuatazo:-
 • Nenda lipa kwa M-Pesa au Tigo Pesa
 •  Chagua lipa kwa M-Pesa au Tigo Pesa
 •  Kisha chagua sehemu ya kujaza namba ya kampuni
 •  Andika namba ya kampuni kwa usahihi ambayo ni 370033
 • Kisha andika namba ya kumbukumbu ambayo utakuwa umetumiwa kwenye ujumbe mfupi (meseji) kupitia simu yako ya mkononi. Ambayo ukirejea mfano wetu hapo juu utagundua kuwa namba ya kumbukumbu ilikuwa ni 213505.
 • Baada ya hapo utapokea ujumbe mara tu ukifanya malipo ukiachana na ujumbe wa Tigo Pesa au M-Pesa utapokea ujumbe mfupi wa maneno (sms) kutoka jatu utakaosomeka hivi; “Hongera malipo yamefanikiwa Bill no AB-2075-SB0001 yenye kumbukumbu na 213505 imefanikiwa kulipwa mzigo utakuja hivi karibuni” Hiyo sms ni kama risiti kwako mteja.

Baada ya taratibu zote hizo utakuwa umefanikiwa kujaza mauzo mwenyewe na pia utaweza kuona gawio lako kama mwanachama. Kumbuka kuwa mfumo huu unakuruhusu pia kununua mara nyingi kadri uwezavyo.

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili