MCHANGANUO WA UWEKAJI AKIBA KWA MSIMU MPYA

RATIBA YA UWEKAJI WA AKIBA YA KILIMO NDANI YA JATU SACCOS LTD KWA MSIMU MPYA WA 2021/2022

JATU SACCOS LIMITED ni chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo kilichoanzishwa na kampuni ya umma ya JATU kilichosajiliwa mwaka 2017 kwa usajiri namba DSR 1655 na mrajis mkoa wa Dar es Salaam wilayani Temeke kwa kufuata sheria za vyama vya ushirika zilizotolewa mwaka 2013 kwa ajili ya kuwawezesha wanachama waliojunga na JATU kushiriki katika fursa za miradi ya kilimo na kujikwamua kimaendeleo kwa kuwapatia mikopo ambayo haina riba na yenye riba riba nafuu kabisa.

Katika kuelekea msimu mpya wa kilimo, JATU SACCOS LIMITED imejipanga kuwawezesha wanachama wakulima kulima bila stress kwa kuwapatia mikopo ya kilimo ambayo haina riba. Katika utoaji wa mikopo hiyo JATU SACCOS LIMITED itazingatia ratiba ya uwekaji wa akiba ya kulimia katika zao husika.

Ratiba hii ya uwekaji wa akiba kwa mazao itaanza mara baada ya mwanachama mkulima kukodi/kununua shamba au kuthibitisha kuwa atalima mwaka 2021/2022. Hivyo mkulima anapaswa kufuata ratiba hii ya uwekaji akiba kila mwezi. Aidha kiwango cha uwekaji wa akiba kimezingatia mwezi husika mara baada ya kuhakiki au kuthibitisha ushiriki wako katika msimu huu 2021/2022.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili