Peter Isare Gasaya
Mkurugenzi Mkuu.

Habari Ndugu Mwanajatu na Mwekezaji Mwenzangu!!

Kwa niaba ya uongozi na bodi ya wakurugenzi wa Jatu ninapenda kukukaribisha kuwekeza katika kampuni yetu ya Jatu inayojishughulisha na miradi ya kilimo, viwanda na masoko.

Jatu ni kampuni ya kitanzania iliyosajiliwa kama kampuni ya umma tangu mwaka 2016 mwezi Octoba tarehe 20 na kupata usajili wa kudumu kutoka BRELLA.

Malengo makuu ya Jatu ni kuhakikisha tunajenga afya na kutokomeza umasikini kupitia rasilimali watu, kilimo na viwanda. Katika kuhakikisha tunatimiza dhamira yetu ya kutokomeza umasikini na kujenga afya,
Jatu tumekuwa tukiendelea kuboresha miradi yetu mbalimbali ikiwemo ile ya kilimo ili kuzidi kuleta tija zaidi kwa wanachama wetu. Jatu imekuwa ikitambua namna miradi ya kilimo inavyohitaji rasilimali fedha na hivyo ili kulifanya zoezi hilo kuwa rafiki kwa wanachama wake kampuni iliamua kuanzisha sacoss yake (JATU SACOSS LIMITED), ambayo ilisajiliwa rasmi kwa lengo la kuwakopesha wakulima wake mikopo nafuu na isiyo na bila riba, lakini pia sacoss hiyo hutoa mikopo midogo midogo ya kimaendeleo yenye masharti nafuu na riba ndogo.

Kupitia miradi ya kilimo kampuni imekuwa ikipata malighafi, huku wanachama wake wakijipatia soko la uhakika la mazao yao ambayo hununuliwa na kampuni kupitia viwanda vyetu ambavyo baadaye huandaa bidhaa za aina tatu, ambazo ni; mchele, mafuta ya alizeti pamoja na unga wa sembe na dona.

Bidhaa zetu zimekuwa zikiandaliwa kupitia viwanda vyetu vya Jatu vilivyopo KibaigwaDodoma na KilomberoMorogoro, huku suala la ubora wa bidhaa hizo likipewa kipaumbele na baadaye kuziuza kupitia mfumo wa masoko yetu ya Jatu (JATU APP). Aidha, mfumo wa masoko ya Jatu, umekuwa ukitoa fursa kwa wanachama wake ambao ni waandaaji wa bidhaa za chakula, usafi na nishati, ambapo kampuni huwatambua kama mabalozi na kuwapatia uwezo wa kuweka bidhaa zao kwenye soko la jatu (JATU APP) na baadaye kununuliwa na wanachama na kupata gawio la faida kila mwezi kutokana na manunuzi yao.

Jatu kwasasa ipo katika mchakato wa kuingia kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (Dar es Salaam Stock Of Exchange), ambapo kampuni imelenga kukuza mtaji na kufikia kiasi cha shilingi bilioni saba na nusu (7,500,000,000/=) ambayo itasaidia kuimarisha viwanda vya jatu hasa kiwanda cha Kibaigwa – Dodoma kinachozalisha unga wa sembe na dona.

Aidha, mtaji huo pia utaiwezesha kampuni kununua zana bora za kilimo na hivyo kufanikisha kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa wanachama wake na watanzania wote wanaoendelea kujiunga jatu. Zipo faida nyingi za kukufanya uamue kununua hisa za Jatu pindi zitakapoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwani Jatu tunaamini hatua hiyo inakwenda kuwakomboa Watanzania wengi kupitia sekta ya kilimo na viwanda, ambapo mkulima atakuwa na uhakika wa kulima bila kutegemea mvua wala kuzingatia msimu, lakini pia uhakika wa kupata mazao ya kutosha kutokana na kutumia zana za kisasa zaidi za kilimo.

Matarajio yetu kama kampuni ni kwamba, ifikapo mwezi March mwaka 2020 tuwe tayari tumesajiliwa katika Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE). Hivyo tunatarajia kuwa utakuwa miongoni kati ya watanzania wengi ambao watanunua hisa zetu pindi zitakapo orodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).

Peter Isare
Founder and C.E.O
Jatu public limited company.
Let money work for you and not you working for money.

Shukrani Sana, Na karibu Sana Jatu.

Jatu tunasema;
“Jenga Afya Tokomeza Umasikini”.