MKUTANO MKUBWA WA WANAJATU KUFANYIKA JUNE, MOSI, 2019


Na: Mwandishi Wetu
Kufuatia kuelekea katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka huu, Kampuni ya Jatu Plc imeamua kuandaa mkutano maalum wa wanachama na umma kwa ujumla mkutano ambao utafanyika ifikapo tarehe 01.06.2019.

 

Akieleza kuhusu mkutano huo, Katibu Mkuu wa Jatu Plc, ndugu; Mohammed Issa Simbano, amesema kuwa, mkutano huo ni muhimu sana na utatumika katika kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya hisa pamoja na umiliki wa mashamba makubwa na ya kisasa kwa gharama nafuu.

 

Aidha, Simbano aliongeza kuwa, agenda nyingine zitakazojadiliwa ni pamoja na mikopo ya kilimo isiyokuwa na riba sambamba na upatikanaji wa soko la uhakika kwa mazao ya wakulima.

 

Pamoja na hayo, ndugu; Simbano amesema kuwa, kupitia mkutano huo uchaguzi wa bodi mpya ya wakurugenzi wa Jatu utafanyika, huku mgeni rasmi wa mkutano huo akitarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh; Felix Lyaniva.

 

Itakumbukwa kwamba, mkutano huo utaanza saa 4:00 asubuhi hadi 9: 00 alasiri na kufanyika katika ukumbi wa ISAMUHYO unaopatikana katika kambi ya JKT MGULANI TEMEKE.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply