MKUTANO MKUU WA WANAHISA WA JATU WAFANA SANA!

Na:Mwandishi Wetu

HATIMAYE Kampuni ya Jatu Plc April 28, 2018 imefanikiwa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo na kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya uendelezaji wa miradi ya kampuni hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Landmark , Mwenyekiti wa Jatu Plc ndugu, Peter Isare amesema kwamba, anashukuru kuona kampuni inakuwa kwa kasi ya ajabu nakongeza kwamba kamwe hakutakuwa na mtu yeyote kuikwamisha kampuni hasa katika malengo ya kufikia ‘ Vision 2022.’

Pamoja na hayo, Isare amewapongeza wanachama wote wakampuni hiyo ikiwa ni pamoja na wanahisa na kusema kwamba, wanachama na wanahisa hao kwa ujumla wao wameifanya kampuni kufika ilipo sasa .

Aidha, Isare amewataka wanachama na wanahisa hao wa kampuni kuendelea kuiamini kampuni na kuwasihi kuendelea kuwekeza zaidi kwa kununua hisa ili kuyafikia malengo ya kampuni kuelekea ‘vision 2022’.

Pamoja na hayo, Mwenyeikiti Isare pia aliutumia mkutano huo kuwasilisha bajeti pendekezwa ya mwaka (2018 – 2022), ambayo iligusa mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya kilimo , viwanda pamoja na masoko.

Mbali na hayo, Isare amesema kwamba, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na kampuni kufikia mwaka 2022 kampuni itahitaji Bilioni 7.5 sambamba na kuboresha miradi mbalimbali inayoendeshwa na kampuni hivi sasa.

Mkutano huo pia ulitoa nafasi kwa wanahisa kufahamu historia ya kampuni ya Jatu kwa ujumla pamoja na kupata ripoti mbalimbali za hesabu za mapato na matumizi kuanzia mwaka 2017.

Pia wanachama wamekubaliana na kusisitiza kwamba mchakato wa kuisajili jatu katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuendelea na kupewa kipaumbele ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki ‘Vision 2022′

Kwa upande wa baadhi ya wanahisa walioshiriki katika mkutano huo wamesema kwamba, wamefurahishwa na namna mkutano huo ulivyo andaliwa vizuri, huku baadhi yao wakiwasihi wanachama wengine ambao bado hawajawekeza kwenye hisa za jatu kufanya hivyo ili kuiwezesha kampuni kusonga mbele zaidi na wao kunafaika pia.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>