MKUTANO WA KILIMO ROBO YA KWANZA, 2022

MKUTANO WA KILIMO ROBO YA KWANZA, 2022

Habari,

NB: “Katika mkutano wa mwisho wa wanahisa uliofanyika tarehe 18.12.2021, wanajatu walikubaliana kuwa na mikutano ya uwekezaji ya mara kwa mara ili kupata mrejesho wa maendeleo ya miradi kwa wawekezaji wake, hivyo kampuni ilikubali uwepo wa mikutano hyo kila robo ya mwaka yaani kila baada ya miezi mitatu” Hivyo basi, Ndugu wanachama na wakulima wote wa JATU PLC mnataarifiwa kuhusu mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka kwa wanajatu wote ambao wanawekeza na wanaopenda kuwekeza katika miradi ya kilimo na ufugaji inayoendeshwa na kampuni katika maeneo tofauti tofauti ya nchi (Tanzania).

Ajenda zifuatazo zitajadiriwa katika mkutano huu;

  1. Mrejesho wa Maendeleo ya miradi ya kilimo Msimu wa 2021-2022.
  2. Mrejesho wa mradi wa ufugaji awamu ya kwanza (Batch 01 – 04) ambayo inaanza kuingia sokoni tarehe 02.04.2022.
  3. Mrejesho wa maendeleo ya malipo ya wakulima wa msimu wa mwaka 2020-2021.
  4. Uzinduzi wa maandalizi na utaratibu wa kushiriki kilimo msimu wa mwaka 2022-2023.
  5. Utararibu mpya wa kushiriki miradi ya ufugaji kwa awamu ya Pili (Batch 05+).

KIINGILIO:
Wote mnaohitaji kushiriki katika mkutano huu mnatakiwa kulipia coupon ya kushiriki kupitia app ya JATU market kwa malipo ya shilingi 25,000/= malipo haya yatajumuisha Tshirt za JATU na nakala ya kitabu maalumu cha msimu wa mwaka 2022 – 2023 ambacho kitapatikana ukumbuni siku ya mkutano.

UKUMBI:
Blue Pearly hotel, Ubungo Plaza, Ubungo, Dar es salaam.

MUDA NA SIKU:
Kuanzia saa 03:00 Asubuhi hadi saa 06:00 Mchana, Tarehe 02.04.2022 siku ya Jumamosi.

“Jatu, Jenga Afya Tokomeza Umaskini”

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili