MUHTASARI PAMOJA NA MAAZIMIO YA KIKAO CHA WAKULIMA WA JATU PLC CHA ROBO YA PILI YA TAREHE 25.06 2022.

Utangulizi

Katibu wa kampuni kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi mtendaji, aliwatambulisha washiriki wote wa mkutano Kwa Makundi na baadae akatoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya kampuni tangu kikao cha mwisho cha wakulima kilichofanyika tarehe 02.04.2022 katika ukumbi wa blue pearly hotel, Ubungo Plaza. Katibu alisema kampuni imepitia changamoto kubwa ambayo kwa kiasi kikubwa imeathiri mfumo wa biashara na hivyo kupelekea ahadi iliyotolewa na kampuni kwa wanachama kuhusu malipo ya madeni yao ambayo yalipaswa kuanza mwezi May hadi December mwaka huu kushindwa kufanyika kwa wakati. Katibu aliweka bayana kwamba Kwa hali ya kiuchumi na mzunguko wa biashara wa kampuni mpango huo hautoweza kutekelezwa kama ilivyokuwa imepangwa na ni kwa sababu hiyo kampuni inalazimika kujadili upya mfumo mzuri wa kulipa na kumaliza kabisa madeni yote ya wakulima kwa misimu yote ikiwa ni pamoja na msimu wa 2021- 2022 ambao mavuno yake yanategemewa kuwa mwaka huu.

Baada ya utangulizi huo wa katibu wa kampuni kukamilika, alimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji kwa ajili ya kutoa mwelekeo mpya wa kampuni.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili