SEMINA ZA MAWAKALA ZIMEBISHA HODI MKOANI MOROGORO

 

 

Semina za mawakala wa Jatu Plc, zimezidi kushika kasi siku hadi siku na sasa ni zamu ya mkoani wa Morogoro baada ya kukamilika huko Visiwani Zanzibar .

Akizungumza kuhusu semina hizo mkoani Morogoro, Afisa Masoko wa Jatu Plc, Mary Richard amesema kwamba, semina hizo zinafanyika mkoani humo katika ukumbi wa kombuna resortukitokea barabara ya sua ‘Round About’ ya kwenda SUA, mbele kidogo kama mita 300 unaingia mkono wa kulia karibu na msikiti wa mahita hapo hapo utakunja kushoto ndipo ukumbi ulipo

Aidha, Mary amesema kwamba, semina hizo zitakuwa zikianza saa mbili kamili asubuhi na hivyo kuwataka mawakala wote wa mkoa wa Morogoro kuzingatia muda huo pamoja na kufika na vitendea kazi vyao ikiwa ni pamoja na ‘Smart Phone’ yenye kifurushi (bando) pamoja na kitabu cha mauzo.

Naye Mkurugenzi wa Jatu, ndugu, Peter Isare amesema kwamba, kutokana na kampuni kudhamiria kutimiza malengo ya mwaka 2022 ipasavyo tayari Kitengo cha Habari, Tehama na Mawasiliano kimeandaa vipeperushi vipya maalum, ambavyo vitatumika kuhamasisha kampeni hiyo ya ‘Vision 2022’ na hivyo kuwataka mawakala na wanachama kufika ofisini ili kujipatia vipeperushi hivyo.

Hata hivyo, semina hizo hazitahusisha mawakala pekee bali kutakuwa na nafasi ya kukutana na wanachama wa kawaida pia, hivyo kwa wakazi wa Morogoro mnahaswa kutopitwa na fursa hii adimu.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>