SIKU YA WALAJI YAADHIMISHWA MTWARA KWA KUZINDUA OFISI MPYA

Na: Mwandishi Wetu

Jana September 08, 2018 kampuni ya Jatu imeadhimisho siku ya walaji (Customer Day) mkoani Mtwara kwa kukutana na wanachama wake mkoani humo na kuwaeleza namna wanavyoweza kuendelea kunufaika zaidi kupitia kutumia bidhaa za kampuni hiyo pamoja na zile za mabalozi wake.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa ofisi mpya na ya kudumu ya kampuni hiyo Mkurugenzi wa Jatu ndugu, Peter Isare amesema kuwa, ofisi hiyo mpya itakuwa ikipatikana katika jengo la PPF ghorofa ya 3 mkoani humo na kuwataka wakazi wa mkoa huo kuitumia vyema ofisi hiyo kwa kupata huduma na bidhaa zote za Jatu.

Aidha, Isare amesema kwamba, Mtwara ni moja kati ya mikoa ambayo wakazi wake wameipokea na kuielewa dhamira ya Jatu kwa kasi kubwa na hivyo kulikuwa kila sababu ya kampuni kuweka ofisi ya kudumu mkoani humo ili kuwahakikishia wakazi hao wanapata vizuri huduma zote za Jatu pamoja na bidhaa zake kwa wakati.

Pia Isare amewahakikishia wakazi wa mkoa huo kuwa, kupitia ofisi hiyo mpya anaamini italeta chachu zaidi mkoani humo na kuwa msaada wa kukuza vipato vyao kutokana na kupata gawio la faida la kila mwezi kutokana na matumizi ya bidhaa zote zinazopatika ndani ya mfumo wa Jatu.

Pamoja na hayo, Isare amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kuangalia namna nzuri ya kufanya kilimo cha pamoja cha zao la muhogo kwa kushirikiana na kampuni, huku akiwataka kuondokana na dhana ya kushindwa wakiwa ndani ya Jatu na kuwataka wakazi hao kuwa mabalozi kwa kutambulisha bidhaa zao katika mfumo wa Jatu.

Mbali na hayo, Kampuni ya Jatu pia imetoa zawadi ya chakula kwa mwezi mzima kwa Bi; Jahida Chande ambaye ni wakala mkoani humo kutokana kufanya vizuri katika kuuza bidhaa nyingi zaidi.

Zawadi nyingine kama hiyo imetolewa kwa Sharifa Mwichande (mwanachama) ambaye yeye ameongoza kwa kuunganisha watu wengi zaidi na kula kilo nyingi za bidhaa.

Naye, Afisa Masoko wa Jatu, Bi; Mary Chulle amesema kuwa, kuanzia sasa wanachama wa Mtwara watakuwa wakipata zawadi za kila wiki kwa mwanachama ambaye ataunganisha wanachama wengi na zawadi za kila mwezi kwa mwanachama ambaye atafanya manunuzi makubwa zaidi.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>