TAARIFA MAALUMU (KILIMO NA UFUGAJI)

TAARIFA MAALUMU (KILIMO NA UFUGAJI)

Ndugu wanachama wawekezaji wa Jatu Plc kwa kutambua umuhimu wa ratiba yetu ya kilimo kwa msimu wa
mwaka 2021/2022 uongozi wa kampuni unatumia nafasi hii kuwatangazia taarifa muhimu kama ifuatavyo:

  1. Tarehe 30.11.2021 ilikuwa mwisho wa kukodi au kununua mashamba kwa mazao yafuatayo: maharage, alizeti na ngano, lakini pia ilikuwa ni mwisho wa kununua mifugo kwa BATCH 01 (BATCH YA KWANZA). Hivyo basi ni muda wa walioshiriki katika miradi hii kuhakikisha wanatimiza vigezo vyote vya miradi hii ikiwamo kuhakikisha umepata risiti zote, umelipia fomu ya miradi,kusaini mkataba na kutimiza vigezo vya Jatu Saccos kwa wanaokopeshwa fedha za kuendesha miradi yao na kuhakiki taarifa zao.
  2. Kwa mwendelezo huo basi, kuanzia tarehe ya leo tunawakaribisha wanachama wawekezaji na watanzania wote kushiriki katika miradi ifuatayo; –
    • Mradi wa kilimo cha maharage ya soya Sumbawanga
    • Mradi wa ufugaji wa ng’ombe na mbuzi kwa BATCH 02 (Batch ya Pili) iliyoanza leo mpaka tarehe 31.12.2021.

Mwisho tunawakumbusha wote wanaotaka kushiriki katika miradi yetu ya Jatu kuhakikisha kwamba wanaweka oda kupitia mfumo wa jatu (JATU APP) inayopatikana kupitia simu yako janja ya kiganjani. Kwa habari Zaidi tembelea tovuti zetu za Jatu, tembelea youtube channel ya Jatu Talk Tv na kurasa zetu kwenye mitandao ya kijamii au fika ofisi ya JATU PLC iliyo karibu na wewe.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili