TAARIFA MAALUMU (KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2021)

TAARIFA MAALUMU (KUELEKEA MWISHO WA MWAKA 2021)

Kwanza kabisa nitumie fursa hii kuwakaribisha katika mkutano mkuu wa 4 wa wanahisa wa JATU PLC utakao fanyika katika ukumbi wa Blue Pearly hotel iliyopo Ubungo Plaza, Dar es salaam tarehe 18.12.2021. wanahisa wote mnaombwa kufika kwa wakati. Baada ya salamu hizo za ukaribisho, Kampuni inatoa taarifa zifuatazo kwa wanachama,

  1. kuanzia tarehe 23.12.2021 hadi tarehe 03.01.2022 tutakuwa katika likizo fupi ya Chrismas na Mwaka Mpya, huduma zote za kiutendaji zitasitishwa hadi hapo tutakaporejea tena kazini. Hata hivyo miradi ya kilimo na ufugaji itaendelea kutekelezwa kama kawaida katika maeneo ya miradi yetu yote
  2. Taarifa ya manunuzi ya mazao ya wakulima ya kipindi cha miezi minne yaani mwezi wa Septemba hadi Desemba tayari imetolewa na kuchapishwa katika (APP) mfumo wa Jatu Talk sehemu ya habari (News) na inaonesha mwenendo wa manunuzi kama ilivyo ahidiwa na uongozi wa kampuni katika mkutano wa wakulima uliofanyika Dar es salaam katika viwanja vya sabasaba maonesho mnamo tarehe 13.11.2021. kampuni itaendelea kununua mazao yaliyobaki na kila mwezi itakua ikitoa taarifa ya mwenendo wa manunuzi.
  3. Wanachama wote wanaoshiriki katika mradi wa ufagaji watembelee APP ya Jatu Talk sehemu ya habari (News) kuona kama taarifa zao zimewekwa katika orodha iliyotolewa, orodha imetolewa kwa wale ambao walifanikiwa kuweka oda (Batch 01) na kukamilisha malipo yao kupitia app ya jatu market, na wote ambao mtakuta taarifa zenu mnatakiwa kukamilisha kulipia gharama za bima na chakula kwa ajili ya mifugo na msaini mkataba wa ufugaji na JATU PLC. Tunategemea kuanzia tarehe 02.01.2022 zoezi la kunenepesha mifugo litaanza rasmi kwa wale ambao watakuwa wamekamilisha vigezo vyote. Kumbuka wale ambao hawajakamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba na JATU, mifugo yao haitaweza kuanza kunenepeshwa. Hivyo tunawaomba ambao taarifa zao hazijakamilika wawasiliane na uongozi wa kampuni ili kukamilisha kwa wakati.

Mwisho tunashukuru na kupongeza wanachama wetu wapendwa kwa kufanya kazi pamoja nasi kwa kipindi chote cha mwaka 2021, tunawatakia kila la kheri tunapoelekea kumaliza mwaka huu na tunawaombea wote mjaliwe afya njema na tuweze kukutana tena katika uwekezaji mwaka 2022. Kumbuka mwaka 2022 ni mwaka ambao tutashuhudia kukamilika kwa JATU VISION 2022.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili