TAARIFA MAALUMU (MKUTANO WA WAKULIMA ROBO YA PILI WA MWAKA)

Habari,
Uongozi wa Jatu Plc unawataarifu wanachama wake wakulima na wafugaji kwamba kutakuwa na mkutano tarehe 25 Juni 2022 kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana katika ukumbi wa mikutano wa Isamuhuyo JKT Mgulani uliopo Temeke karibu kabisa na uwanja wa Taifa wa Benjamini William Mkapa, kikao iko kitakuwa na agenda zifuatazo; –

  1. Kujadili mkakati wa kumaliza madeni ya wakulima Kwa misimu iliyopita pamoja na mavuno ya msimu huu wa 2021/2022.
  2. Kujadili na kuweka utaratibu mpya wa uendeshwaji wa miradi ya kilimo jumuishi katika kampuni.

Tangazo hili linahusisha wanachama tu wanaoshiriki miradi ya kilimo na Ufugaji au mwakilishi rasmi wa mkulima ndio anaepaswa kushiriki mkutano huu, hakutakuwa na kiingilio chochote ili kushiriki mkutano huu. Ahsanteni.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili