TAARIFA MAALUMU (WANACHAMA WOTE WA JATU PLC)

TAARIFA MAALUMU (WANACHAMA WOTE WA JATU PLC)

Habari,
Uongozi wa kampuni unawajulisha wanachama wake na umma kwa ujumla kwamba, kutokana na changamoto iliyojitokeza hivi karibuni, kampuni inafanya mabadiliko yafuatayo; –

  1. Ofisi zote za Matawi ambazo zilikuwa zinatoa huduma za masoko kuanzia jumatatu hii zitafungwa na hazitokua zinatoa huduma hadi pale tutakapo watangazia tena kufunguliwa kwa ofisi hizo. Ofisi zitakazo athirika na mabadiliko haya ni ofisi ya Arusha, Mtwara, Mwanza Na Dodoma. Hata hivyo ofisi za miradi na uzalishaji Yaani kiteto, kilindi, Handeni, Mbingu, Njombe, kibaigwa na sumbawanga zitaendelea kutoa huduma kama kawaida. Huduma zote za kiutawala na masoko zitatolewa ofisi kuu ya JATU PLC iliyopo Dar es salaam, Tanzania.
  2. Kupunguza rasilimali watu katika idara ambazo zinaweza kuhudumiwa kupitia technolojia ya Habari na mawasiliano na hivyo huduma nyingi zitakuwa zikitolewa online.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya. Kwa mawasiliano zaidi tupigie simu +255 (0) 758 396 767.

“Jatu, Jenga Afya Tokomeza Umaskini”

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili