TANGAZO KWA WAKULIMA WA JATU

Habari,

Tunapenda kuwataarifu wanachama wakulima wote ambao waliweka ahadi ya kulipia mashamba kwa msimu wa mwaka 2020/2021, kwamba ifikapo tarehe 15 Septemba 2020 ekari zote ambazo hazijalipiwa zitarudishwa sokoni, ili ziweze kukodishwa na wakulima wengine walio tayari kulipia gharama hizo kwa wakati.

Kampuni inawataka wote walioweka ahadi kufanya malipo hayo kati ya leo hadi Jumatatu, Lakini pia Tunawataka wale wote ambao walikosa nafasi ya kukodi mashamba wawe tayari kukodi mashamba ambayo yatarudi sokoni ifikapo Jumanne ya tarehe 15 septemba 2020.

Ahsante nawatakia Utekelezaji Mwema.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili