TANGAZO MAALUM

 

 

TANGAZO MAALUM

Habari mwanachama wa JATU PLC, tarehe 28.04.2018 katika mkutano mkuu wa wanahisa walipitisha maazimio yafuatayo ili yatekelezwe mapema iwezekanavyo; -

 

 1. Wanahisa watakaoshiriki mkutano wa mwaka wa JATU tarehe 27.04.2019 lazima awe na Hisa 450 au zaidi.
 2. Wanachama wote walio katika mradi wa kilimo kiwango cha chini cha Hisa kiwe 200 badala ya Hisa 50.
 3. Kila mwanahisa ajaze fomu maalumu ya kuahidi ni Hisa ngapi angependa kumiliki JATU, na kwamba atazilipa ndani ya mwaka mmoja (kuanzia tarehe 28.04.2018)
 4. Kila mwanahisa aweke ahadi kununua Hisa zaidi aidha anunue kwa mara moja au aweke utaratibu wa kununua kidogo kidogo kwa siku, wiki au mwezi hadi akamilishe ahadi yake ndani ya mwaka mmoja.

 

 

Lengo kuu la maazimio haya ni kuhakikisha kwamba kampuni inauza hisa millioni tatu (3,000,000.00) zenye thamani ya Tsh. Billioni saba na nusu (7,500,000,000.00) ambayo ndio bajeti ya kampuni kwa mwaka 2018/2019

 

UTEKELEZAJI:

Maazimio haya tayari yameanza kutekelezwa kuanzia tarehe 02.05.2018 na kwamba fomu zitaendelea kutolewa hadi tarehe 31.05.2018 na tarehe 02.06.2018 uongozi utatoa taarifa jumla ya Hisa ambazo zimechukuliwa na wanahisa wa ndani ili kuruhusu hisa zitakazokuwa zimebaki zipelekwe soko la nje (DSE)

 

Kwa niaba ya wanahisa wa Jatu, Mkurugenzi Mkuu anawatakia utekelezaji mwema wa maazimio hayo.

 

Imetolewa na;

Moses Lukoo William

Afisa Habari na Mawasiliano, JATU

Dar es salaam.

04 Mei 2018

2 replies
  • jatu
   jatu says:

   Ina uwezo wa kumsaidia mkulima kulima kisasa na kumfanya kuwa miongoni mwa wakulima bora katika soko la mtandao wa jatu kutokana na mazao yake yanapata soko kupitia JATU pia ukiacha mradi wa kilimo wanachama wenye ubunifu wanafaidika sana na bidhaa wanazobuni ndani ya JATU hawa tunawaita wanachama Balozi katika JATU PLC.

   Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>