TANGAZO MAALUMU

Kampuni ya Jatu Plc imeandaa hafla maalum ya chakula cha jioni kwa wawekezaji nchini Tanzania.
Halfa hiyo imelenga kuwakutanisha wawekezaji mbalimbali nchini ambao watakuwa na utayari wa kuwekeza na kampuni ya Jatu kupitia miradi yake ya kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji.

Mlo huo maalum unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi na serikali kwa ujumla huku, Mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto, Mh. Tamimu Kambona akiwahakikishia wadau watakaoshiriki mkutano huo kuwa, atawaeleza kwa kina fursa zote muhimu zinazopatikana katika halmashauri yake ya Kiteto.
Itakumbukwa kwamba, hafla hiyo itafanyika tarehe 14.03.2020 katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mkurugenzi wa Jatu Plc, Ndugu. Peter Isare.

Pamoja na hayo, uongozi wa kampuni ya Jatu unawakumbusha wadau na wawekezaji wanaotaka kushiriki katika hafla hii kununua coupon mapema kabala ya tarehe 14.02.2020 ili kujiweka katika uhakika wa kushiriki tukio hili la kihistoria nchini.

Kwa msaada zaidi kuhusu namna ya kushiriki halfa hii adhimu unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0657 779 244.

Toa Jibu

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili