VIONGOZI WA JATU SACCOS LIMITED (JSL) WAPATA SEMINA ELEKEZI KUTOKA OFISI YA VYAMA VYA USHIRIKA WILAYA YA TEMEKE

Viongozi wa JSL leo tarehe 20/04/2018 wamekutana na timu ya maafisa ushirika kutoka wilaya ya Temeke ambapo walikuwa wakitoa semina elekezi ya namna ya uendeshwaji bora wa vyama vya ushirika. Maelekezo haya yalitolewa kwenye mkutano mkuu ambapo ulifanyika uchaguzi mnamo tarehe 10/02/2018 ambapo msimamizi wa uchaguzi alielekeza mwenyekiti aandae semina elekezi ambayo ndo imetekelezeka leo.

Kwenye semina hii mafunzo yaligawanyika katika nyanja tofauti kuanzia kwenye maadili ya viongozi,uongozi wa fedha,namna ya kutatua migogoro na pia dhana ya uwekezaji ndani na nje ya saccos kwa masilahi mapana ya wanachama.
Pia maafisa hao wamewasisitiza viongozi kuishi katika maana ya chama cha ushirika kwa maana ya kuwapatia wanachama wake mikopo kwa riba halali na yenye unafuu.

 

Mbali ya semina hiyo elekezi wajumbe wa bodi walikaa kikao cha dharura (ad hoc meeting) na kujadili mambo muhimu kwa afya ya JSL.

Na mwandishi wetu.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>