viwanda

Kampuni ya Jatu inaanzisha viwanda vidogo karibu na miradi yetu ya kilimo, lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa malighafi.

Kupitia viwanda hivyo kampuni hununua mazao ya wakulima ambao ni wanachama wetu na kuandaa bidhaa ambazo tunaziuza kupitia JATU APP kwa mlengo wa masoko ya kimtandao (Network Marketing). Hivyo mwanachama wa Jatu ambaye amelima na kampuni hupata nafasi ya mazao yake kuuzwa katika viwanda vyetu ikiwa ni pamoja na kiwanda cha unga kilichopo Kibaigwa – Dodoma na kile cha Igima, Mbingu wilayani Kilombero mkoani Morogoro amabcho huchakata mpunga na kuongezea thamani, halikadhalika na kile cha kuongeza thamani cha maharage kilichopo Kilindi – Tanga.

Hata hivyo, kampuni ya Jatu imedhamiria kujenga viwanda vingi kadri iwezekanavyo hapa nchini kila wilaya tutakapowekeza kwenye kilimo lazima tuwe na kiwanda maalaum cha kuchakata mazao husika yatakayolimwa katika mradi husika.

Kwasasa kiwanda cha Kibaigwa- Dodoma na Kiwanda cha Mbingu – Morogoro vinaendelea vizuri na kazi na hivyo kufanya kampuni kuelekeza nguvu zaidi katika kiwanda cha Kilindi – Tanga kwa ajili ya maharage.

Aidha, dhamira ya JATUni kujenga kiwanda kikubwa zaidi na cha kisasa wilayani Kiteto mkoani Manyara. Kiwanda hicho kitajikita katika uandaaji wa unga wa dona na sembe pamoja na mafuta ya kupikia ya alizeti.

Kampuni ya Jatu kupitia viwanda vyake hivyo imekuwa ikijivunia ubora wa bidhaa nzuri.

Funga menu
Kiswahili
English Kiswahili