WALIMU WA JATU WAANZA MAFUNZO

Na: Mwandishi Wetu

SEMINA maalum za kuwaandaa watu watakaofahamika kama walimu wa Jatu zimeanza rasmi leo Mei, 03, 2019 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya semina hiyo muwezeshaji mkuu wa semina hiyo ambaye pia ni afisa masoko wa Jatu Bi; Mary Chulle amesema kuwa, lengo la semina hizo ni kuhakikisha kampuni inakuwa na mwakirishi kila eneo ndani ya jijini Dar es Salaam ambaye ataitwa mwalimu wa Jatu.

Aidha, Bi; Chulle amesema kuwa, hao walimu hawataishia kuwa wawakirishi pekee bali watakuwa na jukumu la kuhakikisha jamii za eneo husika wanaifahamu jatu vizuri na kutumia bidhaa na mfumo wa jatu katika manunuzi yao ya bidhaa za chakula, usafi na nishati.

Pamoja na hayo, Bi; Chulle ameongeza kwa kusema kuwa, wawakirishi hao pia watakuwa wakitengeneza kipato kupitia fursa za jatu, hivyo kuwataka wanachama na wasio wanachama ambao wanatamani kuwa walimu wa jatu wafike ofisi kuu za Jatu zilizopo sabasaba maonesho ili kupata utaratibu zaidi.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply