KUJIUNGA JATU PLC

Kwa wote walioelewa kuhusu JATU na wako tayari kujiunga tafadhali wafike ofisini moja kwa moja (Sabasaba Maonesho -Dar Es salaam Au Dodoma Kibaigwa) au kwa wasioweza kufika kwa wakati huu watatuma taarifa zao ofisini kupitia nambari za ofisi ambazo ni +255 (0) 719 292 147 au +255 (0) 744 599 972

GHARAMA ZA KUJIUNGA

Kwa yeyote atakayetaka kujiunga na JATU Plc atatakiwa kujaza fomu maalumu ya uanachama ambayo inapatikana ofisini au kwa mawakala wetu tu ambayo gharama yake ni shilingi elfu Thelathini tu (30,000/=) na atakuwa ni mwanachama wa kawaida mwenye haki ya kununua na kushiriki na kupata huduma zinazotolewa na JATU Plc.

Mara baada ya kusajiliwa na kuwa mwanachama halali wa kampuni, utaruhusiwa kununua hisa kadiri ya uwezo wako ambapo kwa mwanachama wa kawaida kiwango cha chini kununua ni hisa 50 na kwa mwanachama atakayehitaji kuwa wakala wa kampuni atatakiwa kununua hisa kuanzia 400.

Gharama ya hisa moja ni shilingi elfu mbili na mia tano tu (2,500/=).

Kwa mwanachama atakayehitaji kujiunga kwenye kilimo atatakiwa kujaza fomu maalumu ya kilimo ambayo inapatikana ofisini tu kwa gharama ya shilingi elfu ishirini tu (20,000/=) na hivyo kupata fursa ya kushiriki miradi mbalimbali inayohusu kilimo na kusimamiwa na kampuni.

JENGA AFYA TOKOMEZA UMASKINI