WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AWATAKA VIJANA KUIGA MFANO WA JATU PLC

Na: Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu Mstaafu Mh, Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema kuwa ipo haja ya vijana kubadili mitazamo yao kuhusu ajira na badala yake wawaze kujiajiri zaidi kama walivyofanya vijana wa kampuni ya Jatu.

Hayo ameyasema leo tarehe 17.10.2018 wakati alipotembelea banda la Jatu Plc ndani ya Maonesho ya Mwanamke Mjasiriamali yanayofanyika mjini Dodoma kwenye Viwanja vya Nyerere Square, ambapo alisema kuwa “inafurahisha kuona vijana kama hawa jatu walivyoamua kujiajiri badala ya kukaa na kusubiri kuajiriwa’ huku akiwasihi vijana wengine kuiga wengine mfano huo.

Aidha, Pinda alifurahi na namna Jatu inavyowaunganisha wajasiriamali na wafanyabiashara kwa pamoja na kuwapatia soko la uhakika na kusema kuwa ipo haja ya kuangalia utaratibu wa kuwaunganisha pia wazalishaji wa asali ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa hiyo.

Itakumbukwa kwamba maonesho hayo yameanza rasmi leo tarehe 17.10.2018 na yanatarajia kuendelea hadi tarehe 22.10.2018, huku yakihusisha wajasiriamali mbalimbali wa ndani ya nchi na nje ya Tanzania pia.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>