WAZIRI MWIJAGE AWATAKA WAJASIRIAMALI KUTOOGOPA KUZALISHA BIDHAA

Na: Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh, Charles Mwijage amewataka wajasiriamali kutokuwa na hofu katika biashara na badala yake kuhakikisha wanazalisha bidhaa za kutosha.

Hayo ameyasema mapema leo tarehe 18.10.2018 wakati alipokuwa kwenye banda la Jatu Plc ndani ya maonesho ya mwanamke mjasiriamali yanayofanyika mkoani Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere Square, ambapo alisema kuwa bidhaa za chakula ni bidhaa ambazo zinatumika kila siku hivyo hakuna haja ya kuhofia kuzalisha bidhaa hizo za kutosha kwani mara nyingi soko lake si la kusuasua.

Aidha, Mwijage aliongeza kwa kusema kuwa ili kujihakikisha bidhaa za kutosha zaidi ni vyema kulima na kukusanya ili kujihakikishia malighafi za kutosha za uzalishaji wa bidhaa hizo.Jambo ambalo linafanyika pia kupitia miradi ya kilimo ya Jatu.

Itakumbukwa kwamba, maonesho hayo yalianzishwa nchini miaka 12 iliyopita kupitia shirika la kazi duniani ILO na kupitia tamasha hilo shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika kwa lengo la kupanua wigo wa uzoefu na masoko kwenye biashara.

Maonesho hayo ya mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu isemayo ‘Mwanamke mjasiriamali funguka kujenga Tanzania ya viwanda’.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>